Pages

Pages

Saturday, February 09, 2013

Mwanafunzi wa darasa la sita afumaniwa na dereva wa bodaboda

http://api.ning.com/files/Y7XrEGzfaFfHd8wYjo*MnVoljeNXI4K4akiu9hd9qDvKI1a*snHGgLuYpCjNepnAYh6iKZOJgmxAYGAS0KhGXyJe0Ga2EnRB/DENTI.jpg

Mwanafunzi anayedaiwa kufumaniwa (nyuma ya wa kwanza kushoto), akipelekwa shule na ndugu zake baada ya kufumaniwa.

Na Mdakuzi Wetu
ETI kuna tukio la kufumaniwa kwa binti anayesoma darasa la sita aliyekuwa anatoka na dereva wa bodaboda, hivyo mpango wa kumnasa uliandaliwa baada ya kuwekewa mtego.


Tukio hilo lilitokea hivi karibuni na Mdakuzi wetu kujiridhisha na picha za tukio hilo, kabla ya kuwafuata dada zake pamoja na walimu wa shule hiyo lakini walikataa kutoa ushirikiano.

“Utuhoji ili iweje? Swala hili tumelipeleka pale shule na tutalimaliza shuleni kwani hawa wote ni vijana wetu, hatuhitaji habari hizi zitoke kwenye vyombo vya habari,” alisema kwa ukali dada mmoja wa mwanafunzi huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.

Alipotafutwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na kuulizwa juu ya tukio hilo, alikataa kuzungumzia chochote akidai shule yake haihusiki na tukio hilo kwa kuwa lilitokea nje ya maeneo ya shule.

“Sioni sababu ya kutaja jina langu, mimi ni mwalimu mkuu wa shule hii, fumanizi hilo halituhusu kwa sababu halikutokea kwenye madarasa wala vyoo vya shule yetu,” alisema mwalimu huyo.

No comments:

Post a Comment