Pages

Pages

Tuesday, February 26, 2013

Maimatha Jesse: Jamani msinitamani, nimeolewa mieeee



Mdau wa muziki wa dansi, Maimatha Jesse

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANADADA machachari katika sekta ya utangazaji na udau wa muziki, Maimatha Jesse, aliwaacha watu hoi kwa kuwatangazia watu kuwa waache kumuangalia mara mbilimbili kwasababu nafasi zimeisha kwa kusema eti ameolewa.

Kauli hiyo iliwafanya watu waanguwe kicheko wakati mwanadada huyo anazungumzia kuanzisha upya kwa shindano lake la Kigoli wa Extra Bongo na Manywele mwaka 2013, ambalo hadi sasa mipango ya kulitangaza kwa wadau inaendelea.

Huku akirembua macho yake na kubinua barabara mdomo mbele ya hadhira ya waliohudhuria kikao hicho mchana wa leo, Maimatha alishindwa kujizuia na kutamka kuwa yoyote anayemuangalia kwa matamanio ajuwe ameolewa.

“Jamani, ngojeni niwaangalie vizuri nyie wote lakini hadi mwisho mjuwe nimeolewa,” alisema dada huyo ingawa pia hakusema yupo kwenye ndoa na mtu gani.

Hata hivyo kauli kama hii, mwanadada huyo mwenye sura ya mvuto, aliitoa kama sehemu ya kuchangamsha baraza na wala hakuwa na lengo la kujitangaza kwa wadau waliokwenda kusikia kauli ya harakati za Kigoli, akiwa sambamba na Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, mwenye mipango ya kuiweka juu zaidi bendi yake.

Katika kikao hicho, Choki pia alitumia fursa hiyo kumtangaza repa Papy Catalogue, Adam Mbombole na Nadine Conpresor, alijiunga na bendi hiyo akitokea Akudo Impact.

No comments:

Post a Comment