Pages

Pages

Tuesday, February 26, 2013

Clouds FM yakumbwa na rungu la Serikali



Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini ya sh. milioni 5. kwa Clouds FM na kufuta Kipindi cha Jicho la Ng'ombe mara moja kwa kukiuka maadili ya utangazaji.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya, ikiwa ni uamuzi mkali kwa ajili ya kuvifanya vituo vya redio kujiendesha kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

Vituo hivyo Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristo mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment