Pages

Pages

Friday, February 01, 2013

Kinana aendelea kufanya balaa mkoani Kigoma


Katibu mkuu wa chama cha CCM, Abdurahman Kinanan akifungua pazia kuzindua tawi jipya la chama hicho ndani ya kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.


Jiwe la Msingi lililowekwa na Ndugu Kinana.




Ndugu kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi jipya la chama cha CCM kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.



Kinana akisomewa taarifa kutoka kwa wanachama wa chama cha CCM,mapema leo jioni.


Ndugu Kinana akizungumza na wanachama wa chama hicho sambamba na wananchi wa kata hiyo ya Bunyambo,Ndugu Kinana aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kukamilisha ujenzi wa tawi hilo jipa la chama hicho.


Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwambu,Wilaya ya Kibondo,Ndugu Kinana alikwenda shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na pia kushiriki ujenzi wake,pia aliahidi kutoa Solar Pannel kwa ajili ya kuzalisha umeme ofisi za walimu,Kompyuta moja,seti ya jezi mbili sambamba na mipira miwili kwa ajili ya shule hiyo.


Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari ya Kuwambu akiwa sambamba na baadhi wa viongozi wa Wilaya na mkoa kutoka chama cha CCM.


Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya,Wazee pamoja na Jumuiya kwa ujumla wakishangilia jambo kwenye mkutano wao wa ndani uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo.


Ndugu Kinana akizungumza na Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya pamoja na Wazee,lengo ikiwa ni kuwasilisha taarifa ya kazi za chama na serikali,Ndugu Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia shunguli mbalimbali za Vijana sambamba na hilo Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni tatu kwa ajili ya kuwasaidia Walemavu.Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma.


Ndugu Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo,Emmanuel Gwegenyeza,pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Venance Mwamoto pamoja na Kada wa chama hicho,Matoni Nyobeye,mara baada ya kuwasili kijiji cha Kilemba,wilayani Kibondo mapema leo jioni.

Msafara wa Ndugu Kinana pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Mkoa na Wilaya.

No comments:

Post a Comment