Pages

Pages

Friday, February 22, 2013

DC Kilindi aomba minara ya kufanikisha mtandao wilayani kwake



Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa.

Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, amesema ili kuondoa tatizo la ukosefu wa mtandao wilayani kwake, wamefikisha suala hilo katika Wizara husika na kuahidiwa kujengewa minara mitatu katika baadhi ya maeneo yao mapema mwaka huu.
Minara ya simu inavyoonekana pichani.

Akizungumza na Handeni Kwetu mapema wiki hii, Liwowa alisema kuwa bila hivyo maendeleo kwenye wilaya yao yatachelewa kwasababu ya biashara nyingi kuhitaji mtandao wa uhakika, tofauti na hali ilvyokuwa muda huu.

Alisema wananchi na wageni wengi wanaokwenda wilayani humo kwa shughuli mbalimbali, wanalazimika kuishi kwa tabu au kurudi mijini ili wakamilishe kazi zao hizo, jambo ambalo kama wilaya wanakabiriana nalo.

“Dunia ya leo bila kuwa na mitandao ya uhakika huwezi kupata maendeleo ya aina yoyote, hivyo baada ya kuona suala hili, nilijaribu kuzungumza na wenzetu ili watuwekee minara ya kufanikisha huduma za mitandao japo kwa kiasi kidogo tu.

“Unaweza kupiga simu wakati mwingine ukose mtandao, tena wale wanaotaka kutumia kompyuta zao ndio kabisa, hivyo nadhani baada ya kufanikisha suala hilo kutoka kwa serikali kuu, ikiwamo Wizara ya Mawasiliano na ile ya Habari, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Liwowa.

Aidha, matatizo ya mtandao yamekuwa juu kwa wilaya ya Kilindi ambayo imetokana ndani ya Wilaya ya Handeni, tofauti na wilaya ya Korogwe, Muheza na Lushoto ambazo zote zinaunda Mkoa wa Tanga, unaongozwa na RC wake, Chiku Gallawa.


No comments:

Post a Comment