Pages

Pages

Tuesday, February 26, 2013

Ally Choki atangaza kuunga undugu na Villa Squad

Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Next Level, Ally Choki, ametangaza kuunga undugu na timu ya Villa Squad ya Kinondoni na kuapa kufanya nayo kazi kwa ushirikiano.
 
Akizungumza juzi usiku katika onyesho lao kila Jumapili linalofanyika katika viwanja vya Garden Breeze, Magomeni, Choki alisema atasaidiana na Villa Squad katika majukumu yao ya kimichezo.
 
Alisema ingawa Villa wao ni wana soka, lakini haiwezi kuwatenganisha kwa namna ama nyingine, hivyo mashabiki wa bendi yake wanapaswa kuunga undugu huo kwa pamoja.
 
“Nikiwa kama Mkurugenzi wa Extra Bongo, napenda kusema kuwa tutakuwa pamoja na wenzetu wa Villa Squad kwa namna moja ama nyingine, hivyo tudumishe undugu wetu.
 
“Hawa ni wenzetu kwa sekta ya mpira wa miguu na sisi tunafanya muziki, hivyo naomba tuendelee kuwa pamoja kwa kushirikiana pia katika hali ya kuleta mafanikio zaidi,” alisema.
 
Extra Bongo ni miongoni mwa bendi zinazofanya vyema katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, ambayo katika bonanza lake la Garden Breeze Magomeni, limekuwa likajaza watu wengi.

No comments:

Post a Comment