Pages

Pages

Saturday, January 05, 2013

Zitto Kabwe aingia kwenye sanaa zaidi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, amesema ameanza kuifuatilia sanaa baada ya kuona mateso ya ugonjwa wa marehemu Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki, aliyezikwa jana, katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wengi, akiwamo Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Zitto Kabwe, akizungumza jambo katika makaburi ya Kisutu jana.

Zitto aliyasema hayo jana katika mazishi ya Sajuki, akisema kuwa awali hakuingia zaidi katika undani wa masuala yanayohusu sanaa, ingawa sasa anakili kuifahamu vyema kiasi cha kutamani kuingia kwenye mapambano yanayohusu mambo ya sanaa.

“Sikuwa naifuatilia zaidi sanaa, lakini baada ya kuona mateso ya Sajuki, hakika nikaingia kiasi cha kushiriki kucheza filamu ya kuchangisha fedha za kumsaidia marehemu ambaye kwa mapenzi yake amekwenda mbele za haki.

“Nitashiriki kuangalia namna ya kuwasaidia wasanii kwa ajili ya kuweka mambo sawa katika tasnia ya sanaa, maana ina nguvu kama inavyoonekana hapa tunaposhiriki mazishi ya Sajuki,” alisema Sajuki.

Zitto ni miongoni mwa wabunge makini wanaoisumbua sana serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na kutoa hoja nzito kiasi cha kuwasumbua viongozi na watendaji wengi serikalini.

No comments:

Post a Comment