Elizabeth Kilili, Mkurugenzi Grace Products Ltd
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI
na mzalishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka Grace Products Ltd, Elizabeth Kilili,
amesema kwamba changamoto anazokutana nazo sasa ni vifungashio ili bidhaa zake
zionakane katika mwonekano mzuri zaidi.
Elizabeth
aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na Handeni Kwetu, ikiwa ni tamko lake
la kwanza katika kipindi cha mwaka mpya wa 2013.
Alisema
mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha kuwa bidhaa zake, ikiwamo lotion yake Gurlic
and lotion inakuwa nzuri zaidi kwa kuwa na kifungashio kizuri na kinachoficha
mafuta hayo.
“Kama
unataka kufanya biashara kimataifa zaidi, lazima nihakikishe kuwa bidhaa zangu
zinakuwa nzuri kuanzia vifungashio vyake na bidhaa yenyewe kwa ujumla.
“Naamini
mambo yatasaidia kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wa Tanzania tunasonga mbele
zaidi kwa kuhakikisha kuwa tunakabiriana na vikwazo vyotee,” alisema Elizabeth.
Mwanamama
huyo ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Products Ltd, ameingiza sokoni
bidhaa nne, yakiwamo mafuta ya kupaka, sabuni ya kuogea ya Grace Manjano,
Shampooo ambazo zote kwa pamoja zipo chini ya kampuni yake.
No comments:
Post a Comment