Pages

Pages

Friday, January 04, 2013

UDP wamfagilia mbunge Maji Marefu



Mbunge wa Korogwe vijijini, Profesa Maji Marefu

Na Mwandishi Wetu, Tanga.
MBUNGE wa Korogwe vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Ngonyani (Maji Marefu), amemwagiwa sifa na Mwenyekiti wa Chama Cha United Demokratic Party (UDP) Mkoa wa Tanga, Mhina Peter.

Peter amesema Maji Marefu anastahili heshima kutokana na kuchapa kazi bila kuchoka huku akiwa karibu na wananchi wake, hivyo ni mbunge bora kwa upande wake.

Akizungumza leo asubuhi mkoani Tanga, Peter alisema mbali na kuwa karibu na wananchi, pia anatekeleza ahadi zake kwa wakati.

“Kwa maoni yangu Maji Marefu anastahili kuwa bora na huyu ndio mbunge wangu bora kwa mwaka ulioisha, maana amekuwa akishiriki katika juhudi za maendeleo kwa wananchi wake,” alisema.

No comments:

Post a Comment