MGODI UNAOTEMBEA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI ya mkoani Mtwara ni dhahiri inatishia amani, hivyo kuna
kila sababu ya serikali na wadau wote kukaa na kuliangalia suala hilo kwa
marefu.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Nikiwa kama Mtanzania, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu mno
sakata hilo la gesi inayopingwa na wadau kuletwa jijini Dar es Salaam, badala
yake wanataka ibaki mkoani Mtwara, ingawa wenye akili ndogo wanapinga au
kutukashifu kadri ya uwezo wao, wakijidanganya kuwa sipaswi kufuatilia mambo ya
Mtwara na Lindi.
Huu ni udhaifu na hauwezi kuchekewa, maana ni dhahiri
Mtwara, Lindi ni sehemu ya Tanzania kama ilivyokuwa Tanga, Arusha, Kilimanjaro
na kwingineko.
Wananchi hao waliojikusanya kwa ajili ya kupigania sakata
hilo, wamefikia kubadilisha kabisa hisia zao, bila woga wowote katika
kulizungumzia suala la gesi.
Kama nilivyowahi kuhoji hapo nyuma, kuwa tatizo ni gesi,
choyo, siasa au ubaguzi? Makala haya yalitoka katika blog hii ya Handeni Kwetu
na kupokea maoni mbalimbali.
Na haya ndio maoni ya Watanzania hao wanaoishi mkoani Lindi
na Mtwara.
Mwanzo wa ugaidi Tanzania ni mwisho wa amani. Kusini
hawaogopi jeshi.
Kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ipo kwenye mioyo yao. Leo
nasema, ila wana Mtwara watasema kwa sauti zao, maana vitisho kwao ni kama
kuitukana maiti.
Chochote kitatokea iwe ni vita vyovyote vile 2015 hatutaki
uchaguzi na hatutaki pia tuletewe kiongozi na ole wenu, +255712897794.
Kaka nimefurahishwa na makala yako isemayo Tatizo ni ni
gesi, siasa, choyo au ubaguzi? Inaonekana na wewe pia umeandika makala hii kwa
lengo lako binafsi.
Umeshindwa kutoa uhalisia wa jambo lenyewe, badala yake
umeandika kwa lengo la kutaka kumfurahisha ama kuwafurahisha watu fulani.
Rudi nyuma angalia wanachofanyiwa wakulima wa korosho wa
Mtwara je ni sahihi? Lile zao halisaidii kuinua pato la Taifa? Angalia hali ya
maisha ya wakazi wa Mtwara. Nadhani umekurupuka na si mawazo yako kuna mkono wa
mtu nyuma yako.
Nenda kazunguuke na kufanya utafiti wa kina utapata majibu
sahihi kwa wenyeji. +255657614354.
Tatizo la mikoa ya
Kusini sio gesi bali ni kusahauliwa kwa miaka 51 ya Uhuru. Korosho, reli,
Bandari, miundo mbinu, tatizo la elimu na kuwa waanga wa ukombozi wa nchi
zilizopo kusini mwa Afrika.
Wanasiasa kujiingiza katika hoja si ajabu kwasababu duniani
kote wanasiasa ndio huibua matatizo ya wananchi , maana wasomi wetu wengi
hawana meno ya na ndio wanaopitisha mikataba
mibovu .
Sio choyo, lakini tunafikia wakati tunajuta kwa nini sisi
Mtwara Lindi tumekuwa sehemu ya Tanzania. Tuna rasilimali tosha za kuweza
kuitwa, kama vile Bandari, Bahari, Ardhi yenye rutuba, watu, mito, madini, korosho,
ufuta, mhogo na nyinginezo.
Kusini tuna haki ya kumdai mume wetu Tanzania haki zetu za
msingi, maana tumevumilia mno hadi kilio cha kwi kwi. Ni mimi
mwanaharakati, Amoni, wa Kata
Msangamkuu, Mtwara Vijijini. +255652221100.
Ninaomba uelewe lengo la wananchi wa Mtwara na Lindi sio
kwamba hawataki gesi isitumiwe na wengine hapana, wao wanataka kiwanda
kitengenezwe Mtwara.
Kule itoke gesi safi, maana wanakataa mambo yasijekuwa kama
ya madini ya Geita ambayo mwekezaji anachimba anaenda kuhakiki Mwanza na kulipa
kodi ya uwongo na kuiibia nchi na kuwa masikini, huku wakifaidi watu kutoka
nje.
Nimesoma makala yako, inayosema tatizo ni gesi, siasa, choyo
au ubaguzi? Mimi nimeisoma na kwa utafiti wangu, nimegundua kwamba wewe ni CCM
na ndio maana ukaona eti ni siasa. Hapana, ni kwasababu vyama vya upinzani
vinapenda maendeleo ya Watanzania.
Mbona hawakuhamisha miwa kutoka Kagera na kuileta Dar es
Salaam ili itengenezwe hapa? Pili, hebu fikiria gharama za kuweka bomba ni
kiasi gani?
Tatu, kumbuka msongamano mkubwa wa watu, ina maana
wakiongeza viwanda wanazidisha msongamano. Nne, kwanini wasiwaachie watu wa
Mtwara na Lindi na wao wapate ajira?
Tano, kila kilichokuwapo Dar es Salaam, Mtwara kipo kama
vile Bandari na mengineyo. +255713221244.
Ingawa hujaonyesha wazi ujumbe unaopeleka kwa wana Mtwara,
lakini ninachofahamu, Taifa halina rasilimali. Mikoa, wilaya, vijiji, ndivyo
vyenye rasilimali, kama vile mbuga za wanyama, madini, mazao na mengineyo
ambayo mapato yake hukusanywa na kuwa pato la Taifa.
Gesi ni kama rasilimali nyingine tu. Ikiwa Mtwara, Lindi,
Kigoma, Mbeya au popote nchini, tueleze ni vipi italinyima Taifa letu pato? Au
italigawa vipi Taifa? +255717757797.
Hongera bwana Kambi Mbwana kwa makala yako. Endelea kuwapa
elimu Watanzania wenzetu wasioelewa. Naitwa Moi, +255757295249.
Unajua sisi tunaotoka Mtwara tunafananishwa na nyani katika
Taifa hili. Hatuna thamani mbele ya makabila mengine toka Uhuru.
Barabara haijaisha, mazao yetu hayana usimamizi na hatuna huduma
za jamii zilizo bora. Tukipata wakarimu, sio bora pamoja na watumishi wote.
Sisi ni jamii ya mwisho katika Taifa hili, hujiulizi gesi na
mafuta aliyotupatia Mwenyezimungu ingekuwa sehemu nyingine ingehamishwa?
Kwakuwa sisi nyani, hatuna thamani, gesi itaondoka na mafuta
pia yataondoka, maana hawa hawatatuthamini milele. +255712848839.
Asante kwa makala yako, lakini usiwe mwandishi mwoga
anayeogopa watawala walioshindwa kuwaondolea wananchi umasikini na kuligawa
Taifa, kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho. Jitahidi kuwa mkweli ili upate
mafanikio maishani mwako. +255755045295.
Kijana mbona unakuwa kama popo asiyejulikana kama ni mnyama
au ndege. Ya Handeni Kwenu yamekushinda sasa umehamia kwenye gesi.
Nasikitika ujumbe huu uliotumwa kwa namba +255757602075.
nimeufipisha
kwa sababu za kimaadili, maana ulijaa matusi na kashfa kutoka kwa mtumaji,
ambaye pia hakujitambulisha jina lake.
Kaka nimesoma makala zako nyingi, nimegundua wewe ni kada wa
CCM na usiyejua nini wanachokitaka Watanzania.
Hata hujui huko
vijijini watu wanaishi vipi. Unaogopa ya Daudi Mwangosi na Amina Chifupa na huo
sio uzalendo, hivyo hupaswi kuwa mwandishi.
Hivi unajua CCM wanaiendashaje nchi hii? Umeshahoji wananchi
wangapi kuhusu maisha yao badala yake unamfuata Nape Nnauye, unataka CCM ndio
waiongoze nchi milele na milele kwakuwa wewe si mzalendo. Ujumbe huu ulitoka
kwa namba +255652273836.
Nashukuru brother kwa kuweza kupata fursa ya kuweza kusoma
makala yako.
Ni kweli hoja zako ulizozisema zinaweza kushabihiana na
ukweli, ila kutokana na vile hali ilivyo
naweza (kudetermine ya words) nazo yanatokana na siasa pia.
Hebu nambie kaka angu, umaskini uliopo katika mikoa ya
kusini, moja kwa moja tumekuwa maskini na hii ilikua nafasi pekee ya kuweza
kupata ahueni.
Hebu jamani isifike wakati tukawa tunaangalia swala hili
kijuu juu, hali ni mbya kusini hatuna pa kushikia, serikali ilibidi iangalie
gesi hii pia katika kutafuta namna ya kuikomboa miji hii ya kusini.
Ni wazi kuwa serikali imekua ikifurahia tu kupata neema hiyo
kuendesha mambo yao na si kusaidia kuondosha umaskini.
Nyinyi waandishi tunawategemea kutoa hoja za kusaidia
kuondokana na majanga ya kimaskini. Ujumbe huu ulitumwa kwa njia ya barua pepe
kutoka kwa Raya Juma.
Haya ni baadhi ya maoni yaliyoingia mara baada ya kuandika
makala ile, huku watu wakiingia moia kwa moja katika hoja yangu ya siasa,
ubaguzi na choyo nilizokemea.
Kwanini nasema siasa? Ukiangalia hapo, wapo waliotuma ujumbe
huo wakiwa na chukia serikali ya CCM. Hata hivyo, kuyaanika maoni yao si kuwaletea
matatizo, bali kusoma mawazo ya watu wa Mtwara.
Wao ndio wahusika. Ndio wenye kupigania suala la gesi, hivyo
inaweza kuwa njia muafaka ya kuepusha shari inayozidi kujengeka mioyoni mwa
Watanzania, hususan wale wanaoishi mkoani Lindi na Mtwara.
Watu wamekuwa na mawazo tofauti juu ya sakata hilo. Wapo
wale wanaofikia kutamani Mtwara iwe na utawala wake, jambo ambalo hakika si la
kuchekea.
Rasilimali za Tanzania zinaanza kutugawa kadri siku
zinavyozidi kwenda mbele, ndio maana nikaamua kuyaanika mawazo ya ndugu zetu
hao.
Kwa kumalizia tu, sakata la gesi linaweza kujadiliwa upya
kwa kuwashirikisha wadau na wananchi wa Mtwara, hasa kwa kupewa mikakati ya
namna ya serikali kuwapelekea maendeleo maana ni wajibu wao.
Masuala ya chokochoko ya gesi yasiachwe tu kwa wanasiasa
ambao wamekuwa wabunifu kuingia kwenye hoja zinazoshirikisha watu kwa ajili ya
kujijenga kisiasa, jambo ambalo si zuri.
Na sisi tunaofikia kujadili suala la gesi, wakiwamo wana harakati, wasitumie
maneno makali, maana siku zote jazba inaondosha maana husika.
Maoni mengi ya Watanzania nimeshindwa kuyaandika kwa
kwasababu hayajatolewa kiungwana, huku niliyoaandika nikiyafanyia marekebisho
mengi mno.
Katika hili, serikali kwa kupitia Waziri wake wa Nishati na
Madini, Professa Sospeter Muhongo, anapaswa kukaa na kulijadili jambo hili kwa
mapana yake.
+255712053949
+255753806087
No comments:
Post a Comment