Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI inapaswa kuliangalia kwa kina sakata la gesi mkoani
Mtwara na Lindi, kutokana na chokochoko zinazoendelea kutolewa na wananchi wa
mikoa hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Wananchi hao, wamekuwa wakipigania gesi isitoke nje ya mkoa
wao wa Mtwara, wakiwa na nia ya kuhudumia mkoa huo kwa madai kuwa hauna
maendeleo kwa miaka 51 ya Uhuru.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Handeni Kwetu,
walitangaza kuwa harakati zao hazitakoma hadi watakapoona serikali yao
imesikiliza kilio chao.
“Na Tatizo la mikoa ya Kusini sio gesi bali ni kusahauliwa
kwa miaka 51 ya Uhuru. Korosho, reli, Bandari, miundo mbinu, tatizo la elimu na
kuwa waanga wa ukombozi wa nchi zilizopo kusini mwa Afrika.
Wanasiasa kujiingiza katika hoja si ajabu kwasababu duniani
kote wanasiasa ndio huibua matatizo ya wananchi , maana wasomi wetu wengi
hawana meno ya na ndio wanaopitisha mikataba
mibovu .
Sio choyo, lakini tunafikia wakati tunajuta kwa nini sisi
Mtwara Lindi tumekuwa sehemu ya Tanzania. Tuna rasilimali tosha za kuweza
kuitwa, kama vile Bandari, Bahari, Ardhi yenye rutuba, watu, mito, madini, korosho,
ufuta, mhogo na nyinginezo.
Kusini tuna haki ya kumdai mume wetu Tanzania haki zetu za
msingi, maana tumevumilia mno hadi kilio cha kwi kwi. Ni mimi mwanaharakati,” ulisema
ujumbe huo uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Amoni, mwenye
namba +255652221100.
Kwa habari zaidi juu ya sakata hili la gesi na maoni
yaliyotumwa kutoka kwa wadau wa Mtwara na Lindi, usikose kusoma Makala ya Mgodi
Unaotembea kesho Jumatano, Januari 23, katika blog yako ya Handeni Kwetu.
Katika makala hayo, mambo mbalimbali yamejadiliwa kwa kina,
sambamba na kutoa fursa ya kutoa vilio vya wananchi hao waliotuma maoni yao kwa
njia ya simu na barua pepe.
No comments:
Post a Comment