Yusuf Manji, Mwenyekiti wa Yanga
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MFANYABIASHARA maarufu hapa
nchini, Yusuf Manji, ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, amerudisha fomu leo za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa
Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board), huku nafasi hiyo ikiombwa na watu watatu na
uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Februari 22 mwaka huu.
Kama kawaida, Manji alirudisha
fomu akiongozana na mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Zamunda, wakati
waliochukua fomu leo kwa nafasi hiyo ni Hamad Yahya, huku Christopher Peter wa
Moro United na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza, wao wakiomba ujumbe wa
Bodi kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza.
Orodha kamili ya waombaji uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuf Manji wa Yanga wanaoomba uenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Kwa upande wa wajumbe wawili
kuwakilisha klabu za Daraja la Kwanza ni Christopher Peter Lunkombe wa Moro
United ya Dar es Salaam na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza.
Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen ameondoka leo mchana (Januari 18 mwaka huu) kwa ndege ya
South African Airways kwenda Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Ivory Coast na
Morocco zinazoshiriki Fainali za 29 za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazoanza
kesho (Januari 19 mwaka huu) nchini humo.
No comments:
Post a Comment