Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANAMICHEZO 45 wamechukua fomu
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu.
Nafasi zinazowaniwa ni Rais,
Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda 13 tofauti.
Akizungumza leo jijini Dar
es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura,
alisema waombaji wapya 11 ambao ni Richard Rukambura anayeomba urais wakati kwa
upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kaliro Samson, Jumbe Magati, Richard
Rukambura, Omari Walii, Ahmed Mgoyi, John Kiteve, Stanley Lugenge, Francis
Ndulane, Riziki Majara na Hassan Othuman Hassanoo.
Alisema mwisho wa kuchukua fomu
kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10 kamili alasiri.
“Orodha kamili ya waombaji
ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais).
Walioomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib
na Wallace Karia.
“Kwa upande wa ujumbe wa
Kamati ya Utendaji ni Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe
Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na
Vedastus Lufano (Mara na Mwanza,” alisema.
Wengine ni Epaphra Swai na
Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii
(Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu
Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na
Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi, Francis
Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima
(Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange, Hassan Othman Hassanoo,
Riziki Majara na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala, Eliud
Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga)
na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment