Asia Idarous, muandaaji wa Lady In Red
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ONYESHO la mavazi la Lady In Red mwaka huu, limepangwa kufanyika Februari 9 katika viwanja vya Hoteli ya Serena.
Akizungumza na Handeni Kwetu, muandaaji wa onesho hilo na mbunifu Asia Idarous, alisema onesho la mwaka huu litakuwa la tofauti kwa kuwa ni la tisa kufanyika tangu aanze kufanya onesho hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
“Hili litakuwa onesho la kipekee sana, naamini wadau wa mambo ya mitindo watafurahia na hata maandalizi yameanza kukamilika,” alisema Asia.
Wabunifu mbalimbali wamitindo hapa nchini wanatarajiwa kuonesha mavazi yao, baadhi ya wabunifu hao ni Ally Remtula, Mustafa Hasanali, Khadija Mwanamboka, Gymkhana, Salimu Ally, Catherine Mlowe na Vyone Peter.
Wengine ni Dayana Magese, Rukia Walele, Jackson Gumbala, Lucky Creation, Naima Masika Hamidi Abdul, Ailinda Sawe na Annete Ngogi.
Pia Asia aliwataja baadhi ya wadhamini wa onesho hilo kuwa ni Darling Hair, Redds, Vayle Spring, Kebbys Hotel, One Touch Solution, I View Production, Packeting Africa, Nyumbani Entertainment na Nyumbani Lounge.
No comments:
Post a Comment