Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema kuwa mwamuzi
Sylvester Kirwa, kutoka Kenya,
amepangwa kuchezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na
mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Handeni Kwetu jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa TFF,
Boniface Wambura, alisema mwamuzi huyo anatambuliwa na Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA).
Mwamuzi huyo atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range,
huku waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.
“Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya
Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa
Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina
yake,” alisema Wambura.
Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa inasubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa soka, ikiwa ni siku chache baada ya timu ya Taifa,
Kilimanjaro Stars, kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya Chalenji,
iliyomalizika nchini Uganda.
No comments:
Post a Comment