Pages

Pages

Sunday, December 16, 2012

‘Subiri kwanza nilale’, kauli chungu kwa mwanaume


MAMBO FULANI MUHIMU

Wapendanao wakifurahia penzi lao
 
Na Kambi Mbwana
NYUMBA hizi zinaficha mambo mengi mno. Bila hivyo watu tungekuwa tunatembea huku siri zetu zikiwa nje, maana yote yanajulikana.

Nasema hivi kama utangulizi wangu wiki hii katika makala haya ya Mambo Fulani Muhimu, ambayo hakika yana wapenzi wengi nje na ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Ndio, maana wapo watu hasa wanawake hawapendi kujishughulisha, huku uvivu ukiwasumbua sana, kiasi cha kuwaudhi waume zao.

Ni pale wanapoombwa na waume zao, wawape haki ya ndoa, huku wao wakiwawekea ngumu. Hawataki kabisa kwa kisingizio kwamba wamechoka.

Wengine husingizia usingizi, wakitaka walale kwanza hadi watakapoamka. Hali hiyo ni mbaya sana. Maana wanaume ndio huwaumiza zaidi.

Wao wanapotaka haki hiyo ya ndoa, huwa wameshafika hisia, jambo ambalo kwakweli ni gumu. Kwa bahati mbaya, akina mama hao wanaosema kwanza walale, hawawezi kuamka wenyewe hadi watakaposumbuliwa upya.

Hii ni mbaya kwakweli. Inawatesa na kuwasononesha wenzao, ndio maana baadhi yao huchoka hivyo kuamua suluhisho pekee ni kuwa na wapita njia.

Wale ambao hawataki waambiwe, maana wanajua fika njia ya kwanza ya kumteka mwanamume ni kumlaghai, kumpa raha ya ndoa hadi achanganyikiwe.

Nafikiri hili ni jambo ambalo tunatakiwa tuliangalie upya katika hali ya kuboresha ndoa zetu ama uhusiano wetu. Jua kabisa mikono yako ndio inayoweza kuvunja ndoa yako ama uhusiano wako kwa mwenzako.

Huna budi kuwa makini kwa nia ya kuhakikisha kwamba ndoa yako inaendelea kuchanua na sio kusambaratika kwa ujinga wako unaosumbuliwa na uvivu.

Ni wepesi sana kusema “nimechoka bwana ngoja kwanza nilale hadi nitakapoamka”Kauli hii ni nzuri kwao, ila ni mbaya kwa wenzao.

Hasa inapotolewa kila siku, kama njia ya kumnyima mwenzake haki ya ndoa. Nasema haki ya ndoa kwa wale waliobarikiwa na Mungu juu ya jambo.

Wanamume hao wanachukizwa na mambo hayo, wakisema yanawaumiza wao, hasa wanapohitaji haki yao, ukizingatia kwamba hata dini imeruhusu.

Sawa, dini imeruhusu kwa wale walioingia kwenye ndoa, hivyo sidhani kama yupo mwanamke ambaye anaweza kukataa tu ali mradi amkomowe mume wake.

Hiyo siyo tabia nzuri hata kidogo. Mnapokerwa na tabia mbaya ya uhuni wa wanamume wenu, pia mcheze kwenye nafasi zenu kwa kuziba ufa huo wa umalaya.

Mwanamume asiyetosheka kwa mke wake, hakika ana nafasi kubwa kutoka nje ya ndoa. Huo ndio ukweli. Wewe ambaye hii ni tabia yako kuwa makini.

Unapaswa kujua kiasi gani mtu wako anahitaji dozi zako, ndio maana ameamua kuwa na wewe. Na kama hutaki tena, mpe sababu za kueleweka, lakini sio usingizi.

Huo ni umbea. Usingizi unakujaje katika dimbwi hilo la mahabati. Acha hizo wewe. Nani anaweza kusinzisia hapo? Labda wewe, lakini mwenzako hawezi kulala, eti kwasababu wewe umemwambia ulale kwanza.

Yeye atalala macho. Akikusubiria uinuke ili umpe haki yake ya ndoa. Wasi wasi ni kwamba kuna siku utainuka, wakati yeye ameshawasha gari na kwenda kwa madada poa wanaojiuza ili apumzishe maumivu yake.

Utajisikiaje utakapoletewa magonjwa ya zinaa kwasababu ya ujinga wako? Jiulize mwenyewe, maana hakika wewe ni tunu ndio maana mwanamume wako ameamua kuwa na wewe, hivyo lazima uwe makini.

0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment