Pages

Pages

Monday, December 24, 2012

Simba B: Viongozi Simba wameoza

 Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
SAKATA la kuondoka kwa kocha wa timu ya vijana ya Simba, Selemani Matola na meneja wake, Patrick Rweyemamu, limeingia sura mpya baada ya Rweyemamu kusema kuwa uongozi wa klabu hiyo umeoza na hawawezi kuongoza kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo ya klabu yao.

Rweyemamu aliyasesema hayo mapema leo, akielezea kusikitishwa kwake na mwenendo wa Simba iliyoambulia nafasi ya tatu katika mashindano ya vijana mwaka huu.

Akizungumza na Handeni Kwetu mapema leo mchana, Rweyemamu alisema kwamba viongozi wa Simba hawana jipya na wameshindwa kabisa kuongoza kwa ushirikiano.

Alisema kwamba wameshindwa kuiandaa timu pamoja na kutoa walau fedha ndogo za nauli, huku wakiwa wepesi kushangilia matokeo ya ushindi uwanjani.

“Hii ni mbaya kwa timu kama Simba inayoangaliwa na kila mmoja wetu, hivyo nadhani suala hili haliwezi kuibeba timu yetu ndani na nje ya nchi ikiwamo hiyo ligi ya Mabingwa.

“Viongozi hawapo makini na ndio maana kwa pamoja tumeamua kujiondoa katika timu, huku nikiwataka kuacha kupotosha umma kuwa wametuondoa klabuni,” alisema.

Timu ya vijana ya Simba B, imeambulia nafasi ya tatu, huku ubingwa ukienda kwa timu ya Azam FC, wakati mshindi wa pili imechukuliwa na Wagosi wa Kaya kutoka Tanga, Coastal Union.

No comments:

Post a Comment