Pages

Pages

Saturday, December 22, 2012

Samatta, Ulimwengu wazomewa uwanjani

Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta

Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya mashabiki wa soka wa Tanzania, walitumia muda mwingi kuwadharau na kuwakejeli nyota wa timu ya Taifa, Taifa Stars, katika mechi iliyowakutanisha Stars na Zambia, katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki.

Mechi hiyo ilipigwa katika Uwanja wa Taifa, huku Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakishindwa kuingia uwanjani kutokana na kuwa wanaumwa.

Vijana hao wawili wanakipiga katika timu ya TP Mazembe ya nchini Kongo, huku nyota zao zikiwaka kupita kiasi, jambo linalowafanya waishi kama wafalme.

Tabia ya kuzomewa haijaanza leo, kwani John Bocco, naye aliwahi kuingia kwenye sakata hilo hadi kutangaza kuachana na timu ya Taifa, hata hivyo wadau na viongozi wa soka walimtaka mshambuliaji huyo kupuuza mashabiki anapokuwa uwanjani.

Zomea hiyo inatokana na baadhi ya wadau wa soka kufikiri kuwa nyota hao wanaokipiga Kongo hawana mapenzi na timu ya Taifa, kitu ambacho bado hakijatibitishwa na kutoka kwa daktari wa timu hiyo.
 
Katika mchezo uliomalizika hivi punde, Samatta na Ulimwengu hawakuingia uwanjani zaidi ya kukaa benchi wakiangalia wenzao wanavyoipeperusha Bendera ya Taifa.

Bao pekee na la ushindi liliwekwa kimiani na Mrisho Ngassa katika mechi iliyokuwa na ushindani wa aina yake, huku Christopher Katongo, akishindwa kuleta madhara kwa Stars, licha ya kuogopwa na mabeki wengi Afrika.

Bao la Stars liliwekwa kimiani na Ngassa katika dakika ya 45, huku mechi hiyo ikichezeshwa na mwamuzi kutoka Kenya, Sylvester Kirwa.

Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Kapombe, Aggrey Moris, Kelvin Yondan, Frenk Damayo, Amri Kiemba, Abubakar Salum, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Khamis Mcha.

Zambia ni Danny Munyao, Chintu Kampamba, Hichan Himonde, Chisamba Lungu, James Chamanga, Moses Phiri, Christopher Katongo, Felix Katongo, Nanthan Sinkala, Roderick Kabwe na Isaac Chansa.

 

 

No comments:

Post a Comment