Pages

Pages

Tuesday, December 25, 2012

Heri ya Krismasi muungwana



Heri ya Krismasi
 
Na Timu ya Handeni Kwetu
LEO Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla inaadhimisha Sikukuu ya Krismasi, ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kwa sababu hiyo basi, Handeni Kwetu inachukua fursa hii kuwatakia Wakristo wote duniani sikukuu njema.

Handeni Kwetu tunaomba msheherekee kwa amani Sikukuu hii pamoja na kukumbuka walau mstari mmoja wa kwenye kitabu Kitukufu cha Biblia iwe kama faida kwenu kwa siku ya leo duniani.

Pia muitumie Sikukuu hii kuwaombea wengine wenye matatizo ili Mungu awape furaha na amani mioyoni mwao. Zile nchi zenye vurugu za kidini basi kadhia zao hizo zikome kutokana na dua zinazoelekezwa kwao.

Yale mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi yazidi kuzikumbuka nchi masikini kwa kuwapa mikopo isiyokuwa na masharti magumu yanayosababisha kuvunja uaminifu wa pande zote mbili.

Kwa kuyasema hayo, tunaamini leo ni siku nzuri kwa watu wote, huku ikiwa bado siku tano tu mwaka huu kumalizika na kuingia 2013 kama uhai baaadhi yao tutakuwa nao.

Asanteni sana kwa kuinga mkono blog hii ya Handeni Kwetu, huku tukiamini kuwa tutaendelea kuwa bega bega kwa bega na nyie kwa kuwaletea habari mbalimbali pamoja na makala zilizoandikwa kwa kina, ikiwamo siasa, michezo na nyinginezo.

+255  712 053949
+255 753 806087

No comments:

Post a Comment