Pages

Pages

Sunday, December 09, 2012

DC Handeni ataka watu wawekeze kwenye kilimo



Picha ya juu, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akiangalia zao la mananasi lilivyostawi, katika shamba la SISIMUA Estate, lililopo Kwamsisi. Picha inayofuata ni migomba wakati ya chini ni DC akimuangalia mbwa katika shamba hilo.


MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesema kwamba kuna haja ya wananchi wa Handeni kuwekeza zaidi kwenye kilimo badala ya kuwaachia wageni au matajiri na kuwaachia ardhi zao kwa bei ya kutupwa.

Muhingo aliyesema hayo juzi alipotembelea shamba la SISIMUA Estate, lililopo katika kijiji cha Kwamsisi, akiwa na baadhi ya wanafunzi kutoka shule za Kwamsisi, Kwalugulu na Handeni Mjini, katika lengo la kujifunza masuala ya kilimo cha kisasa.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Muhingo alisema kilimo ndio uti wa mgongo, hivyo watu wajiingize humo kwa ajili ya kujitafutia maisha yao, badala ya kuuza ardhi zao kwa bei ya kutupwa, wakati wangeweza kujiendeleza kimaisha.

“Huu sio muda wa kuacha kulima na kuwaachia wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa sisi tunakuwa hatuna cha kufanya, hivyo nadhani Watanzania wote pamoja na watu wa wilaya yangu tungezinduka sasa.

“Naamini tukifanya hivyo, mambo yatakuwa mazuri ukizingatia kwamba tuna ardhi kubwa na yenye rutuba, ndio maana wageni wanakuja kwa wingi kwa nia ya kuwauzia mashamba wakati tunaweza kulima wenyewe na kuinua maisha yetu,” alisema Muhingo.

Muhingo aliitumia siku ya Jumamosi ya Desemba 8 kuzunguukia katika vijiji mbalimbali vya Kwamsisi kwa nia ya kuangalia changamoto za wananchi, ikiwamo elimu na kilimo, haswa kwa kutembelea pia shamba la kisasa.


No comments:

Post a Comment