Pages

Pages

Friday, December 07, 2012

DC Handeni aapa kukaza mkanda zaidi



Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akizungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake

Na Kambi Mbwana, Handeni
MKUU wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesema kuwa kamwe hataogopa vitisho wala kutokuungwa mkono katika harakati za kuingoza wilaya ya Handeni na kufikia malengo aliyojiwekea.

Muhingo aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake jana, akielezea mikakati na changamoto anazokutana nazo katika utendaji wake wa kazi, ukiwamo msimamo wake wa kuhakikisha mabinti wanakwenda shule.

Akizungumzia suala hilo, Muhingo alisema kwamba watu wanaodhani kuwa atapunguza makali yake wanajidanganya, badala yake ataendeleza harakati zake zaidi kwa ajili ya kuwakomboa kielimu mabinti kutoka kwa wazazi wasiojitambua.

Alisema ingawa zipo changamoto anazokutana nazo, lakini amekuwa akifanya vikao na kukutana na baadhi ya watu, akiwa na le ngo la kuwaweka sawa na kuonyesha kuwa nguvu anazotumia hazitapungua zaidi ya kuziongeza kwa kufanikisha malengo yake.

“Sitapunguza makali bali nitaongeza zaidi hivyo wanaojidanganya kuwa nguvu hizi zitapungua wanajidanganya, maana lengo hapa ni kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu pamoja na wale wazazi wasiowapa watoto wao nafasi ya kusoma.

“Kazi bado ninayo kubwa sana, hivyo naamini kadri ya uwezo wangu nitaifanikisha kwa kutetea kile ninachopenda kifanyike na sio kupunguza kasi yangu, hasa katika suala la elimu ambalo ndio muhimu na mtaji kwa siku za usoni,” alisema Rweyemamu.

Rweyemamu ni miongoni mwa wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni na kuingia kwa kasi sana katika maeneo yao ya kazi, huku akisimamia na kuendesha zoezi la kuwakamata wanaowapa mimba au wazazi wanaowaozesha mabinti zao na kuwaachisha masomo katika sehemu mbalimbali za Wilaya ya Handeni.

No comments:

Post a Comment