Pages

Pages

Tuesday, December 18, 2012

Chimwemwe atamkoma Francis Cheka



Francis Cheka

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka, amepangwa  kurudiana na Chiotra Chimwemwe wa Malawi, Januari 26, nchini Ethiopia.

Pambano hilo litapigwa katika jiji la Adddis Ababa, likitoa picha na kutangaza makali ya Mtanzania huyo, mwenye asili ya mkoani Morogoro kasoro bahari.

Akizungumzia juu ya pambano hilo, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC), kwa kupitia Rais wake, Onesmo Ngowi, alisema pambano hilo litafanyika mara baada ya kumalizika lile la jijini Arusha, lililopangwa kufanyika Desemba 26.

Alisema Cheka na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG).

“Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja kwa ajili ya kuonyeshana umwamba,” alisema Ngowi.

Umaarufu wa wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka katika patashika hiyo.

No comments:

Post a Comment