Pages

Pages

Friday, September 30, 2011

Wimbo wa kazi ya dukani





 Dogo Mfaume huyu akiwa katika pozi


Haiiii ya ya ya ya yaaaa ohoooo
Ohoooo yayaya ohoooo
Hii kazi yangu ya dukani mimi naona inalipa
Nikizingatia zitaweza filisika
Baba kabla ya kufa, alinipa usia
Mwanangu kazi ya kufanya fungua duka
Eheeeee funguu duka
Na ukizingatia hutaweza filisika
Sasa wanakijiji wamepanga wanitimuwe
Jamani ndugu zangu nipeni ushauri wa bure
Niache kuuza duka au nifuge nguruwe
Hiyo haiwezekanii
Hiyo ni tofauti tambi na mboga ya majani
Kama wanamuziki Yondo na Marijan
Yote mimi najua sababu demu wa Fulani
Yeye akija kwangu dukani
Analeta sana matani
Hii yote najua sababu demu wa fulani
Yeye analeta sana matanii
Anajiona yeye ndio bora
Mali hazina thamani
Kumbe hana lolote anataka kunilaghai
My Dogo mafi me Peace&Love
Yani namaanisha upendo na amani
Kaka mkanye mkeo atalala kwenye majani
Eheeeee kazi ya dukani mieeeeee
Naona inaniweka matatani


Kiitikio

Kazi yangu ya dukanii eheee inaniweka matatani
Ehee kazi yangu ya dukaniii ohooo inaniweka matatani
Eheee wanaonirudisha nyuma wengi wao majirani
Majiraniiii, wanaonirudisha nyuma wengi wao majiraniii
Majiranii, wanaonirudisha nyuma wengi wao majirani

Ubeti 2

Aiiiiiiii yayayayayayayayayaayayayaa ohooo
Ohoooooo, yayayaa ohooo
Yani kila kukicha mi naona masiara
Baada ya miezi sita sitakuwa na biashara
Sasa nimekata mtaji wangu wa sigara
Ilikuwa juzi mimi na bwana Sele
Alipokuja dukani nimkopeshe mchele
Anataka kilo mbili watoto wake wakale
Nitafanya nini mimi nitafanya nini
Naogopa kugombana na majirani
Nikitazama duka langu linakata
Siku zote hakuna ninachopata
Haina kulia mi nabaki tu kucheka
Kwani tayari duka lishafilisika
Na hivi sasa, nimeshachoka
Hivi sasaaa nimeshachoka
Zege nabeba, kokoteni nasukuma
Debe napiga shamba la mtu nalima
Yamenijaa moyoni nashindwa hata kusema
Ningekuwa nyoka sumu ningezitema
Marafiki wameshiriki, kunifilisi
Mpaka sasa wote mimi nawaona nuksi
Wameleta mikosi juu ya mikosi
Na kazi yangu ya dukani imeniweka matatani
Nikikumbuka mi napatwa na simanzi
Maumivu ya moyo hayapoi kwa ganzi
Hayaaa ohooo yayayaaaaa ohooo

Kiitikio

Kazi yangu ya dukanii eheee inaniweka matatani
Ehee kazi yangu ya dukaniii ohooo inaniweka matatani
Eheee wanaonirudisha nyuma wengi wao majirani
Majiraniiii, wanaonirudisha nyuma wengi wao majiraniii
Majiranii, wanaonirudisha nyuma wengi wao majirani

Yapu yapu yapu yapu pruduce welter
Hii ni sauti ya mwanao
Yule yule Dogo Mfaume
Angalia haooo, watakufilisi
Wasikope kimbizaaaa haooo
Haruna Moshi Boban
Professional Players
Wapi Juma Nyoso
Yanini utumbo utupwee
Wakati wenyewe twalia ndizi
Ahaaa producer maneno yako haya
Mkurugenzi Peter

No comments:

Post a Comment