Pages

Pages

Thursday, September 29, 2011

Masikini Sinta weeeeeeeeee







 Juma Nature juu akiafutiwa na mwanadada Sinta wakati picha ya chini na Nature na mke wake. Na hapo ndipo pabaya, maana sidhani ndoa yake itadumu endapo uhusiano huo utaanza upya.

NYOTA wa filamu aliyewahi kutamba katika kundi la Kaole Sanaa Group, Christina Manongi, maarufu kama Sinta, yupo kwenye wakati mgumu akifikiria zaidi uhusiano wake mpya na Juma Kassim, Juma Nature, aliyewahi kuwa na uhusiano naye.

Hata hivyo mwanadada huyo hajaweka wazi uhusiano huo na Nature, zaidi ya kusema kuwa anafikiria kama anaweza kufanya naye kazi ya sanaa, hususan filamu na muziki.

Sinta, anayefanya kazi katika kampuni ya mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, ameweka wazi hisia hizo na kuonyesha kuwa anaumwa na kichwa kwa kumuwaza mkali huyo wa ‘Wanaume Halisi’, licha ya kusema kuwa haamini kama anaweza kufanya naye kazi bila kinyongo chochote.

Licha ya kupendana wakati huo, wawili hao waliingia kwenye mkwaruzo mkubwa uliosabibisha Nature atunge vibao viwili vya kumsema mwanadada huyo.

Nyimbo hizo ni ‘Sitaki Demu’ na ‘Inaniuma Sana’, akiweka bayana hasira zake juu ya binti huyo aliyetingisha vikali katika vyombo vya habari kutokana na urembo wake.

Vibao hivyo vilifanya vema mno katika vituo vya redio na kuzidi kumuweka juu mkali huyo mwenye bahati kubwa.

Mara baada ya mwanadada huyo kuweka hisia zake kwa baadhi ya marafiki zake, wengi walionyesha wakimuuanga mkono kwa wazo lake na kumtaka asahau na kumpokea tena Nature, kama anataka kufanya naye kazia huaku akiambiwa kuwa itafanya vema.

Sinta alikuwa kimya kwa muda mrefu tangu alipogombana na Nature, kitu kinachowafanya baadhi ya watu washikwe na hamu ya kuwaona wawili hao wakiwa pamoja.

1 comment:

  1. Kaaazi kwelikweli! yangu macho ..nje ya mada nimestuka kiduchu nilipoona hilo jina SINTA ..maana kuna watu huwa wananiita hivyo...

    ReplyDelete