Na Mwandishiwetu, Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewaasa vijana wa Zanzibar kuwa Wazalendo na
nchi yao kwa kuisoma na kuijua historia
ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati
Sheikh Abeid Amani Karume.
Dkt.
Shein ameyasema hayo wakati akitoa
hotuba ya ufunguzi katika kongamano la
kwanza la kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa
Baraza la mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere katika kampasi ya
Zanzibar, iliyopo Bububu mjini Magharibi
siku ya Alhamis tarehe 5 April, 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya
ufunguzi wakati wa kongamono la kumbukumbu ya hayati sheikh abeid amani karume
lililoandaliwa na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere kampasi ya zanzibar.
“Hayati
Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa ni mtu mvumilivu na mstahimilivu,
aliyeipenda Zanzibar na wananchi wake, hivyo ni vyema mchango wake katika
kuleta maendeleo ya Zanzibar ukakumbukwa na kuenziwa.
Rais Karume ametumia fursa hiyo pia
kukipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuona umuhimu wa kuandaa
Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika visiwani Zanzibar.