Pages

Pages

Tuesday, April 03, 2018

Watanzania waaswa kuchangamkia makazi nchini Oman

Meneja Mauzo Mwandamizi wa  Kampuni ya Ujenzi wa Makazi ya Muriya, Ghizlane El Gouchi (wa pili kushoto) akiwaonyesha wageni waliohudhuria hafla ya kuitambulisha kampuni hiyo kuelekea maonyesho ya biashara yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam hadi Aprili 5 na Zanzibar Aprili 6. Kushoto ni Mshauri wa Mradi Mona Abel Malak, mshauri mwandamizi, Faisal Alzakwani,Mshauri Hamad Al Balushi na mshauri mwingine Omar Saleh. 

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Watanzania wameaswa kuchangamkia nyumba zinazouzwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake Muscat nchini Oman, ili kujiweka katika kundi sahihi la kibiashara sanjari na kujipatia maendeleo makubwa kutoka kwa nchi ya Tanzania na Oman.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko na Kampuni ya Muriya Ghizlane El Gouchi, wakati anazungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nyumba zinazouzwa na kampuni yao huku maonyesho hayo yakifanyika jana katika Hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wenye ndoto za uwekezaji wa majengo.

Maonyesho hayo yaoiendelea leo jijini Dar es Salaam leo latina Hoteli ya Hyatt.

Alisema kwamba Tanzania na Oman ni nchi mbili zenye uhusiano mkubwa wa kindugu na kibiasharaa, hivyo ni wakati wa Watanzania wenye ndoto za kuwa wafanyabiashara wakubwa, kujitokeza kwa wingi katika uwekezaji wa majengo yanayotolewa na kampuni yao pembeni mwa viwanja vya Golf na pembezoni mwa bahari.

Muriya ni kampuni kubwa iliyojikita katika utoaji wa huduma za makazi na utalii nchini Oman, ambao tumeingia katika soko la Tanzania baada ya kufanikiwa pia kwenye soko la ndani, tukiamini kuwa ni wakati mzuri wa kutoa fursa za makazi kwa Watanzania wote.

 “Taratibu za malipo ni rahisi kwa sababu mtu atakayekuwa tayari kununua, anakuwa na fursa ya malipo kwa awamu nane ndani ya miaka miwili ambapo mteja atalipia asilimia 10 mara baada ya kujisajili na asilimia 10 ya mwisho ni atakapokabidhiwa, huku gharama zetu zikianzia Dola 98,000 tu,” Alisema El Gouchi.


Kwa mujibu wa El Gouchi, mradi wao wa Jebel Sifa ni mwendo wa dakika 40 tu kutoka Muscat, karibu na ufukweni ambayo yana ukubwa hadi wa square meter 365,000, ukiwa ni mradi mkubwa unaowahusu Watanzania wote na ni fursa nzuri za uwekezaji.

Maonyesho hayo ya kibiashara ya makazi yanayouzwa na Kampuni ya Muriya mbali na kufanyika jijini Dar es Salaam, Hyatt Regency Hoteli kuanzia tarehe  Aprili 3 hadi 5, pia yanatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar Aprili 6 Park Hyatt Hoteli kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni kwa ajili ya kuendeleza kutoa elimu juu ya fursa hizo za makazi inayotolewa na Muriya, kampuni iliyoanzishwa nchini Oman.



No comments:

Post a Comment