Pages

Pages

Friday, December 29, 2017

Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano








Kutoka Kushoto  Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanziabar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni mwalikwa, Kaimu  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio mji wa Jeddah Bw. Salim Ali Shatri.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wa Jeddah wakiwa katika picha na meza kuu baada ya mkutano.

Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia ' Tanzania Welfare Society' hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza. Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni rasmi. Mhe. Pandu Amir Kificho alikuwa nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada ya 'Umrah' katika miji ya Makkah na Madina.

Wanajumuiya walipata fursa ya kusikiliza hotuba zilizotolewa na Balozi na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi. Vile vile waliweza kuuliza maswali na pia kutoa maoni na ushauri. 
Katika hotuba zilizotolewa wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania. Habari zimeletwa na Mwandishi Maalumu wa Jeddah, Saudi Arabia. Kwa Picha na matukio mengine zaidi angalia youtube kupitia 'Prince eddycool' 
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident.

Wednesday, December 13, 2017

Serikali yaipongeza Bikosports kuijaza mapesa Stand United


*Waziri Mwakyembe asema mpira ni pesa
*Ataka wadau wengine wawekeze

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, chini ya Waziri wake, Mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe, ameipongeza Kampuni ya Bikosports kwa kitendo chake cha kuidhamini timu ya Stand United ya Shinyanga kwa Sh Milioni 100.
Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe, akiangalia jezi yake aliyokabidhiwa na wadhamini wa klabu ya Stand United ya Shinyanga, Bikosports, wakiwa kwenye tukio la klabu hiyo kukabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 100 kama sehemu ya udhamini kwao. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bikosports, Charles Mgeta, akiwa sambamba na Mbunge wa Shinyanga Mheshimiwa Steven Masele na kulia ni Mwenyekiti wa Stand United, Dr Ellyson Maeja.

Serikali imetoa kauli hiyo leo katika makabidhiano ya hundi ya Sh Milioni 100, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Akemi na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa serikali, viongozi wa TFF na wadau wengine muhimu wa michezo.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mwakyembe alisema duniani kote mpira ni pesa, hivyo kitendo cha Kampuni ya Bikosports kuamua kuidhamini Stand kutachochea ari ya mafanikio katika nyanja ya mpira wa miguu nchini.

"Serikali inawapa hongera Bikosports kwa kuingia kwenye mpira wa miguu, hivyo ni matumaini yetu nitaongeza wigo wenu wa udhamini sanjari na kuingia pia kwenye klabu nyingine, tukiamini sasa mpira utachezwa uwanjani, hivyo Stand United lazima waitumie vizuri fursa ya kupata mdhamini," Alisema.