Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Shilingi Milioni 20 za Biko kutoka kwenye Bahati
Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Anthony Chitanda, amekabidhiwa fedha zake
mapema jana katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es
Salam, sambamba na kupewa ushauri wa kifedha.
Chitanda aliibuka kidedea katika droo ya 30 ya Biko
iliyochezeshwa juzi Jumatano na kuvuna Sh Milioni 20 zinazotolewa na
waendeshaji hao wa Biko, mchezo wa kubahatisha unaoendelea kutingisha katika
wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Bahati Nasibu ya Biko, Hassan
Melles kulia amkabidhi mshindi wao wa droo ya 30 Anthony Chitanda
katikati katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Afisa wa NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika jana mchana.
Akizungumza katika Makabidhiano hayo, Mratibu wa Matukio na
Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema kwa kila anayecheza bahati nasibu
yao, lazima ajiandae kulala masikini na kuamka tajiri.
Alisema ushindi wa Biko ni rahisi kwa wale wanaocheza kwa
kutumia mitandao ya simu ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo namba ya
Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea Biko
kikianzia Sh 1,000 na kuendelea.
Mshindi wa droo ya 30 Biko Ijue Nguvu ya Buku, Anthony Chitanda kushoto akiwa na mke wake baada ya kukabidhiwa hundi ya fedha zake Sh Milioni 20 saa chache kabla ya kuelekea benki ya NMB, Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhiwa fedha zake jana.
“Mbali na kushinda Sh Milioni 20 kama alivyoshinda Chitanda
na hatimae kumkabidhi fedha zake siku moja baada ya kushinda, pia Watanzania
wanaweza kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000,
50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku wanaocheza mara nyingi zaidi
kwa kufanya miamala kwenye simu zao wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda
zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na
Jumapili kwa ajili ya kuwania donge nono la Sh Milioni 20,” Alisema.
Naye Chitanda alisema kwamba fedha za Biko ni tamu inapotokea
bahati ya ushindi, huku akisema amekubaliana na kauli mbiu ya Biko
inayojulikana kama ushindi nje nje, kutokana na kuibuka kwake mshindi wa Sh
Milioni 20 ambazo amekabidhiwa haraka.
“Nimekubaliana kwa kiasi kikubwa na kauli mbiu hii ya ushindi
nje nje, maana awali nilijua sitaweza kushinda, lakini kwa kushinda kwangu,
naomba niwaambie Watanzania wote waendelee kucheza Biko washuhudie nguvu ya
Buku inavyozalisha mamilioni,” Alisema Chitanda.
Baada ya kukabidhiwa fedha zake pamoja na kupewa ushauri wa
kifedha kutoka kwa wataalamu wa NMB, mshindi mwingine wa Biko wa Milioni 20
anatarajiwa kupatikana Jumapili hii kwenye droo ya 31.
No comments:
Post a Comment