Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20, mshindi wao wa droo ya 28, Moses
Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa jana Jumatano, jijini Dar es Salaam.
Moses Matagili mshindi wa Biko wa Milioni 20 mkazi wa Goba, katikati
akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko,
Hassan Melles kulia, huku akishuhudiwa na afisa wa NMB, tawi na Bank House,
jijini Dar es Salaam leo mchana.
Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa
kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za
M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya
kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili
anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake
kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa
Biko.
Mshindi wa droo ya 28 ya Biko, Moses Matagili, kushoto
akipokea fedha zake jumla ya Shilingi Milioni 20 kutoka kwa Mratibu wa Matukio
na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB leo jijini Dar
es Salaam.Mshindi wa Biko wa Milioni 20, Moses Matagili akiwa anafurahia fedha zake saa chache baada ya kukabidhiwa leo katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.
Alisema makabidhiano hayo ya fedha yamefanyika haraka,
tofauti na matarajio yake, ikiwa ni siku moja baada ya kupigiwa simu ya ushindi
na Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
“Nashukuru kwa kushinda na kukabidhiwa fedha zangu mapema,
nikiamini kuwa nitapiga hatua kubwa kiuchumi kwa namna moja ama nyingine,
ukizingatia kuwa ndio matarajio yangu.
“Nawaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko mara nyingi
zaidi na wasikate tamaa, kwa sababu kushinda kwangu kumeniongezea imani kubwa
kwa waendeshaji wa Biko,” Alisema.
Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan
Melles, alisema Biko inaendelea kutoa fedha mbalimbali kuanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa papo
hapo kupitia simu za washiriki waliocheza Biko.
“Biko tunaendelea kulipa fedha mbalimbali za papo kwa hapo
pamoja na droo kubwa ya Jumatano na Jmapili ambayo ni Sh Milioni 20, kama
tulizompa leo mshindi wetu wa Goba,” Alisema Melles huku akiwataka Watanzania
waendelee kucheza Biko ili waibuke na zawadi mbalimbali.
Wakati mshindi huyo akipokea fedha zake, tayari mshindi wa
droo ya 27, Viane Kundi, mkazi wa Iringa Mjini naye akiwa ameshapokea fedha
zake Jumatatu iliyopita, huku pia mwezi Mei na Juni pekee Biko wakiwa
wameshatoa zawadi zaidi ya Sh Bilioni moja.
No comments:
Post a Comment