Pages

Pages

Tuesday, July 04, 2017

Mkuu wa wilaya Kibaha awapogeza washindi wa Biko


Na Mwandishi Wetu, Kibaha

MKUU wa Wilaya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama, amewapongeza washindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ na kuwataka kuweka umakini na malengo katika fedha zao wanazokabidhiwa ili wanufaike kiuchumi.

Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama katikati wakati wa kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 19 ya Biko, Elisiana Laizer kulia mwenye gauni jekundu ndani ya benki ya NMB, Tawi la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

DC Asumpter ameyasema hayo jana katika tawi la NMB, Mlandizi, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 zilizokabidhiwa kwa Mshindi wa droo ya 19, Elisiana Simon Laizer, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, mwenye maskani yake Mlandizi, aliyeibuka kidedea katika droo ya 19 ya bahati nasibu hiyo ya aina yake inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu za mikononi za Tigo, Vodacom na Airtel.


Akizungumzia bahati nasibu hiyo ya Biko, DC Mshama alisema michezo ya kubahatisha ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wao na uchumi wa Taifa kwa kuhakikisha kwamba wanafanya shughuli zenye kuleta maendeleo badala ya kuzitumia kwa mambo yasiyokuwa na msingi.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama kulia akimkabidhi jumlaa ya Sh Milioni 20, mshindi wa Biko droo ya 19, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, Elisiana Laizer, mwenye maskani yake Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama wa pili kutoka kulia, akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Biko wa Sh Milioni 20 aliyepatikana katika droo ya 19, mkazi wa Mlandizi, Elisiana Laizer kulia kwake mwenye gauni jekundu. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven na mmoja wa watendaji wa juu wa benki ya NMB kwenye tawi la Mlandizi.


“Nimeshuhudia kwa macho yangu umekabidhiwa fedha hizi Sh Milioni 20 kutoka kwa watu wa Biko, hivyo nitaanza kukufuatilia hatua kwa hatua ukizingatia kuwa upo katika wilaya yangu na mimi kama DC nimekuja hapa kushirikiana na wananchi ili tupige hatua kiuchumi,” Alisema DC Mshama.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha zake, Elisiana Laizer alisema mbali na kuwa ni mjasiriamali wa kuuza sabuni, lakini hatakuwa na papara katika matumizi ya fedha zake alizokabidhiwa baada ya kushinda Biko droo ya 19, huku akiwa ni mchezaji mzuri wa mchezo huo.


“Nashukuru kwa kupewa fedha hizi lakini kwakuwa ni nyingi sana, nitatuliza akili yangu badala ya kufanya papara katika kuzitumia, maana ndoto yangu ni kuhakikisha kuwa fedha zinakuza uchumi wangu, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu tucheze Biko ili tuweze kuibuka na ushindi wa droo kubwa ya Sh Milioni 20 ya Jumatano na Jumapili,” Alisema.


Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kuendelea kuchangamkia mchezo wao ili waweze kuvuna donge nono la Jumatano na Jumapili pamoja na kuzoa zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama ya mchezo ikianzia Sh 1000 na kuendelea na ukichezwa kwa kutumia simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.


“Leo tumemkabidhi mshindi wetu wa Mlandizi sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka kwa wataalam wa benki ya NMB wa tawi la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku ikiwa Biko imeendelea kutoa ushindi kwa wachezaji wetu wa mikoa mbalimbali ya Tanzania, hivyo tunaomba Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi zaidi ili waweze kuibuka na mamilioni ya Biko,” Alisema Heaven.


Kwa miezi miwili tangu kuanza kwa bahati nasibu ya
Biko, Biko imetoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi katika miezi miwili ya Mei na Juni, ikiwa ni njia ya kuwanufaisha wachezaji wao hapa nchini.

No comments:

Post a Comment