Pages

Pages

Wednesday, June 21, 2017

Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiwa kwenye tukio la kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 16 ya Biko, ambapo bwana Ramadhan Hussein wa Dodoma aliibuka kidedea na kuzoa kiasi hicho cha pesa kutoka Biko. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DONGE nono la Sh Milioni 20 la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 16, leo limeenda kwa mshindi wao Ramadhan Juma Hussein, mwenye maskani yake mjini Dodoma, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Makao Makuu ya Nchi ya Tanzania kupata mshindi wake katika droo kubwa inayofanyika Jumatano na Jumapili.

Ushindi wa Ramadhan umekuja siku chache baada ya kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, aliyekabidhiwa pesa mapema wiki hii.
Akizungumza katika droo hiyo leo mchana, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alimpongeza Ramadhan kwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20, huku akiwataka Watanzania wote kucheza kwa wingi na mara nyingi ili wazoe mamilioni ya Biko.

“Naomba kutangaza kwamba mshindi wetu wa Jumatano hii wa Sh Milioni 20 ni Ramadhan anayetokea mjini Dodoma, ambaye pia amekiri kucheza Biko mara kwa mara pamoja kuwahi kushinda zawadi za papo kwa hapo ambao zinatoka kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinatoka kila dakika kwa wale wanaocheza bahati nasibu yetu.

Mchezo huu unachezwa kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye mitandao ya simu ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel, ambao huingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, baada ya kufanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea na kupata nafasi ya kuwania zawadi za papo kwa hapo bila kusahau kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20,” Alisema Kajala.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Biko imezidi kukolea baada ya kumpata mshindi wa Dodoma kwa mara ya kwanza tangu waanze kuchezesha bahati nasibu yao, huku akiwapongeza wote waliowahi kushinda donge nono la Biko kutoka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.

“Ni furaha kubwa kuona Dodoma wameibuka na donge nono la Biko, huku nikiamini kuwa kucheza Biko ni rahisi pamoja na kuweza kuibuka na ushindi wa zawadi za papo hapo bila kusahau zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka mara mbili kwa wiki,” Alisema Heaven.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za uwapo wa bahati nasibu ya Biko, akisema kwamba ni rahisi kucheza pamoja na urahisi pia wa kuibuka na ushindi.

“Uwapo wa mwakilishi wa Bodi kwenye droo ya Biko unatokana na dhamira ya kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa, hivyo niwatoe hofu Watanzania kuwa Biko ni mchezo halali unaofuata sheria zote za nchi,” Alisema Ndaki.

Mara baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika jana, jijini Dar es Salaam, Biko itamkabidhi mshindi wao huyo wa Dodoma jumla ya Sh Milioni 20 kwa ajili ya kuziingiza kwenye majukumu yake ya kimaisha, huku dalili za kupanua biashara zake kuwa kubwa baada ya kutangaza kwamba ni mjasiriamali wa simu mkoani Dodoma.



No comments:

Post a Comment