Pages

Pages

Monday, June 26, 2017

Milioni 20 nyingine za Biko zaenda tena Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA hali inayoonyesha ya kuchachamaa na kuchangamkia fursa, droo ya 17 ya Bahati ya Nasibu ya Biko ‘ijue Nguvu ya Buku, imefanyika jana jijini Dar es Salaam, huku fundi charahani wa Mjini Dododoma, Evodi Mlingi, kuibuka kidedea na kujinyakulia jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na Biko.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza na simu ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Dodoma, Evodi Mlingi aliyepatikana baada ya kuchezesha droo ya 17 ya Bahati Nasibu ya Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki.

Droo ya kumtafuta mshindi huyo wa Sh Milioni 20 imeendeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Mlingi ni mshindi wa pili wa anayetokea Dodoma mjini kujinyakulia Sh Milioni 20, akitanguliwa na Ramadhan Juma Hussein, aliyekabidhiwa fedha zake wiki iliyopita.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, akiandika dondoo baada ya kupatikana kwa mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 17 ambapo Evodi Mlingi mkazi wa Dodoma aliibuka kidedea. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

 
Alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza na rahisi pia kushinda kwa kutumia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh 1,000 na kuendelea huku namba ya kampuni wakipaswa kuingiza 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Huu ni wakati wa kutajirika kwa kupitia Biko, hivyo tunampongeza mshindi wetu wa Dodoma, Mlingi kwa kushinda dodo la Sh Milioni 20, huku nikiwakumbusha kuwa kila mtu anaweza kushinda zawadi mbali mbali za fedha taslimu za papo kwa hapo kuanza Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washindi,” Alisema.

Naye mshindi huyo wa Dodoma, Mlingi aliwashukuru Biko kwa kumtangaza mshindi katika droo ya 17, huku akisema sasa maisha yake yamekuwa mazuri kwa kuzitumia vizuri fedha za bahati nasibu hiyo atakazopewa.

“Nilikuwa nacheza Biko kwa malengo ya kushinda, hivyo leo kutangazwa mshindi hatimae ndoto zangu zimetimia, maana pamoja na kucheza sana, pia nilikuwa namuomba Mungu anipe nafasi ya mimi kushinda ili niimudu familia yangu,” Alisema kwa hisia fundi charahani huyo kutoka Dodoma Mjini.

Kwa upande wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, aliwapongeza Watanzania wote wanaojitokeza kwa wingi kucheza Biko akisisitiza kuwa ni eneo zuri la kunufaika kuichumi kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.
“Watanzania wacheze kwa wingi kwa sababu ni mchezo unaofuata vigezo vyote kutoka kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, nikiamini kuwa wanaweza kujikomboa kiuchumi kwa kupitia fursa ya michezo hii ya kubahatisha hapa nchini,” Alisema.

Kwa kutangazwa mshindi kwenye droo ya 17, sasa Mlingi anajiandaa kupokea fedha zake haraka iwezekano kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu hiyo ambao Mwezi Mei pekee waliweza kutoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa washindi wao.



No comments:

Post a Comment