Pages

Pages

Sunday, June 11, 2017

Mkazi wa Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam aibuka na Milioni 20 za Biko

Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kulia akiwa kwenye majukumu ya kumtafuta mshindi wa droo ya 13 ya Biko ambapo kijana mwenye miaka 23 mkazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam, Amani Kabuku, alifanikiwa kuibuka na zawadi nono ya Sh Milioni 20. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya 13 ya Biko waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha Tanzania maarufu kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, imefanyika leo asubuhi, huku mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaa, Amani Kabuku, mwenye miaka 23, akifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh milioni 20.

Mshindi huyo ameibuka katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Akizungumza katika droo hiyo leo asubuhi, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema ni wakati wa kutajirika kwa kupitia mchezo wao wa Biko uliozidi kujizolea umaarufu katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.
Kajala Masanja kulia akizungumza huku akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Alisema anaamini washindi wao wanaoendelea kujipatia fedha mbalimbali kupitia mchezo wao, huku akiwataka Watanzania waendelee kucheza kwa kufanya miamala ya fedha kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000, ambapo namna ya kucheza ni kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

“Wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri yaushindi wa zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zikilipwa moja kwa moja kupitia simu zao za mikononi walizotumia kuchezea Biko,” Alisema Grace.

Naye Balozi wa Biko Kajala Masanja aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kucheza Biko ili wajipatie chanzo kipya cha uchumi ili wajiendeshe kiuchumi.

“Huu si muda wa kuachia wengine wajipatie fedha huku wengine tukikaa tu, badala yake wote tuamke ili kuchangamkia fursa ya kiuchumi kwa ajili ya kupata mtaji kwa ajili ya kujiendesha kimaisha kwa namna moja ama nyingine,” Alisema.

Akizungumzia ushindi wake, mshindi huyo kutoka Mbezi, Amani  aliwashukuru Biko kwa kumtangaza mshindi utakaompatia jumla ya Sh Milioni 20 ambazo zitamsaidia kwa kiasi kikubwa katika vitu vitakavyomuwezesha kiuchumi.

“Nashukuru kwa kutangazwa mshindi wa Biko wa droo ya 13 ambayo kama nikipata fedha hizo Sh Milioni 20 hakika nitazitumia vizuri katika kuinua kipato change, ukizingatia kuwa nilicheza Biko kwa malengo ya kushinda kwa kumuomba Mungu,” Alisema Amani.

Kwa kutangazwa mshindi huyo, Biko wanatarajia kumpatia zawadi yake mapema wiki hii kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anaziweka katika matumizi yake ya kuinua uchumi wake, huku mamilioni mengine yakiendelea kutoka kwa ushindi wa papo kwa hapo pamoja na Sh Milioni 20 kwa droo ya Jumatano hii.


No comments:

Post a Comment