Pages

Pages

Tuesday, June 13, 2017

Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, akiwa katika furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSHINDI wa Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ wa  droo ya 13, Amani Kabuku, jana amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa zawadi hiyo ya donge nono itamkomboa kiuchumi, licha ya umri mdogo aliokuwa nao, akiwa na miaka 23 tu.


Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.
Mshindi  wa Sh Milioni 20 wa droo ya 13 ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, katikati akiwa amepakatia fedha zake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyekamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mshindi huyo na kuingiza pesa zake. 

Akizungumza kwa furaha kubwa, mshindi huyo alisema ndio kwanza amemaliza kidato cha sita na kuibukia kwenye fedha hizo za Biko, hivyo anaamini zitamkomboa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maisha yake yanakuwa mazuri.

Mshindi wa Sh Milioni 20 katikati Amani Kabuku, akisaidiwa kushika 'maburungutu' yake ya fedha baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.

Alisema amecheza mara nne tu kabla ya kutangazwa mshindi katika droo ya 13 iliyofanyika Jumapili iliyopita, ambapo hata hivyo hakuamini haraka hadi alipowaona baadhi ya wafanyakazi wa Biko walipomfuata nyumbani kwao kwa ajili ya kumhakikishia juu ya ushindi huo. 

“Ni furaha kubwa niliyokuwa nayo kwa sababu naamini huu ni wakati wa kuaga umasikini maana wengi wanatafuta nafasi kama hii ambayo leo Mungu ameniletea mimi ili niweze kutimiza ndoto zangu katika umri niliokuwa nao, hivyo nawashukuru Biko, huku nikiwataka Watanzania wacheze kwa wingi ili nao washinde kama ilivyokuwa mimi,” Alisema Kabuku. Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kutumia fursa ya uwapo wa mchezo wa bahati nasibu ya Biko ili washinde zawadi nono kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kwa ushindi wa papo kwa hapo, ambapo bahati nasibu yao ikichezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456. 

“Baada ya kuingiza namba ya kampuni kinachofuata ni kuweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi, huku wale wanaocheza mara nyingi wakiwa na nafasi kubwa ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili, ambapo Jumapili hii mshindi mwingine wa Sh Milioni 20 akitarajiwa kupatikana katika droo kubwa,” Alisema Heaven.


Kwa mwezi Mei pekee, bahati nasibu ya Biko imeweza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wake wa papo kwa hapo pamoja na wale walioibuka na droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili, huku wakiamini kuwa uwapo wa mchezo wao wa kubahatisha ukiwa ni njia ya kukuza uchumi kwa washiriki wao na Watanzania kwa ujumla, huku pia ukiwa ni mchezo rahisi kuliko michezo mingine yoyote inayofanyika nchini Tanzania.


No comments:

Post a Comment