Na Anthony John, Globu ya Jamii
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Muhidin Sufiani.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango yao kwa wakati.
Sanjari na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945 wamechangia na wamepewa na ya usajili.
Hata Hivyo Mweketi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya Tanzania ya Viwanda iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani wafanyakazi watakapo kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na kuleta Maendeleo.
No comments:
Post a Comment