Na Mwandishi
Wetu, Arusha
HALMASHAURI
ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, jana imepokea kompyuta mbili zilizotolewa
msaada na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya
ushirikiano na kusaidia na kukuza ufanisi wa kikazi kwa watumishi wa umma
wilayani humo.
Kompyuta
hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaada
kama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa katikati akizungumza jambo katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Kulia ni Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Emelda Kisosi.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo leo jijini Arusha, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial
Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya
hiyo kama orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta hizo.Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.
Mercy Mgongolwa akikabidhi nyaraka za kompyuta hizo.
“Huu ni
mwendelezo mzuri wa ugawaji wa kompyuta 205 tulizonunua zenye thamani ya Sh
Milioni 500, ambapo tayari kompyuta 125 zimefikishwa Makao Makuu ya Utumishi na
wao kutuelekeza eneo na idadi ya ugawaji kwenye halmashauri za nchi yetu,”
alisema.
Naye Afisa
Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Imelda Kisosi, aliwashukuru Bayport
kwa kujitolea vifaa hivyo muhimu vitakavyowapatia urahisi watendaji hao kuchapa
kazi kwa nguvu zote ili wilaya yao isonge mbele.
“Msaada huu
ni mkubwa mno kwetu hivyo tunawashukuru na kuwaahidi ushirikiano wa hali ya juu
sanjari na kuwataka Bayport waendelee kuwa karibu na jamii yetu kama njia ya
kuwapatia maendeleo Watanzania wote, hususan wa wilayani kwao Arumeru, mkoani
Arusha,” alisema Kisosi.
Bayport Financial
Services ni taasisi ya mikopo inayojitolea kwa hali na mali ambapo mbali na
kununua kompyuta hizo 205, pia imekuwa ikishiriki kujenga madarasa katika shule
mbalimbali, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kupanua kiwango cha elimu
nchini.
Huduma znazotolewa
na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na
wafanyakazi wa kampuni binafsi, mikopo ya viwanja, mikopo ya fedha kwa njia ya
simu za mikononi maarufu kama ‘Nipe Boost’, Bima ya Elimu kwa Uwapendao na
nyinginezo zinazopatikana katika ofisi zao za matawi 82 katika mikoa na wilaya
mbalimbali za Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment