Pages

Pages

Thursday, November 03, 2016

Teknolojia imerahisisha maisha ya binadamu duniani

Na Jumia Travel Tanzania
Miaka kadhaa iliyopita kabla ya matumizi ya tekinolojia kuingia na kushika kasi mtu ulikuwa ukitaka kusafiri itakubidi kuulizia kwa watu ambao tayari wameshawahi kuwepo kwenye eneo unalolitarajia kwenda.

Baadae kidogo simu zilivyoanza kuingia zilirahisisha mambo watu wakawa wanapigiana simu na kuulizana hali na mazingira kwa ujumla ya eneo wanalotaka kwenda ili kujiandaa vema.

Lakini sasa hivi kwa msaada wa tekinolojia ni wewe tu aidha na simu au kompyuta yako iliyounganishwa vizuri na mtandao wa intaneti ambapo unaweza kupata taarifa lukuki bila ya kumuhusisha mtu yeyote yule. 

Kadiri ya maendeleo ya tekinolojia yanavyokua sehemu mbalimbali duniani na ndivyo huduma mbalimbali zinavyosogezwa na kurahisishwa zaidi kumzunguka binadamu.

Leo hii mtu huna haja ya kupata shida ya kuanza kusumbuka kutembea umbali mrefu au kumuuliza jirani, ndugu au jamaa kuhusu huduma kama vile za usafiri, malazi, bidhaa, na bei zake kwani kila kitu kimo na kinaweza kupatikana kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Vivyo hivyo kwa upande wa huduma za usafiri na utalii zilivyorahisishwa na mitandao ya huduma za hoteli kama vile Jumia Travel, Expedia, Airbnb, TripAdvisor, Booking.com na kadhalika.

Wasafiri na watalii wengi wa siku hizi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wanapenda kupata huduma wazitakazo kwa urahisi zaidi na uhakika wakiwa mahali popote.

Wanataka kwamba wakiingia kwenye mtandao aweze kupata taarifa zote juu ya sehemu anayotaka kwenda kama vile atafika kwa njia gani pamoja na sehemu atakayofikia.

Kwa upande wa malazi mitandao iliyotajwa hapo juu imekuwa na nafasi kubwa sana katika kuhakikisha msafiri anapata sehemu ya uhakika anayoihitaji, gharama na hadhi yake.

Mitandao hii inatoa uwanja mpana wa kuweza kupata huduma zote sehemu moja, za uhakika tena ndani ya muda anaoutaka msafiri.

Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo ilimbidi mtu afanye taratibu za malazi kwa sehemu anayokwenda mpaka atakapofika.

Kwa namna moja ama nyingine mitandao hii ya huduma za hoteli kwa mtandao na tekinolojia kwa ujumla imeleta msaada mkubwa na mapinduzi ya hali ya juu kwa watoa huduma nchini na sehemu zingine duniani.

Licha ya maendeleo hayo na madhumuni mazuri ya tekinolojia katika kuboresha maisha ya binadamu lakini bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji hususani wasafiri kuiamini na kuitumia mara kwa mara lakini pia hata kwa wenye hoteli na sehemu zingine zinazotoa huduma za malazi kwa ujumla.

Bado wasafiri wengi wanaamini kuwa huduma za kweli na uhakika utazipata mara utakapofika eneo husika licha ya kuwa kwenye mitandao hii kuna picha, huduma, gharama na mawasiliano ya wahusika.

Na kwa upande wa wamiliki wa sehemu za malazi kama vile hoteli bado nao hawana imani kubwa na wamiliki wa hii mitandao. Wao wanadhani kwamba wanaweza kutumia hoteli zao kuwatapeli wateja na kunufaika wao binafsi, dhana ambayo si kweli.

Ukweli wa mambo ni kwamba kwa watumiaji wa huduma hizi, wateja na wamiliki wa hoteli ambao huitumia mara kwa mara wamethibitisha imekuwa na msaada mkubwa sana.

Kwa mfano, hoteli nyingi hutegemea umaarufu wa sehemu husika ndio mteja aende na kutumia huduma zao kitu ambacho kwa dunia tuliyopo na tunayokwenda nayo kinapitwa na wakati.

Kupitia mitandao hii wamiliki wa hoteli na sehemu zingine za malazi wana wigo mpana wa kuwapata wateja kutoka maeneo mbalimbali kwani huduma zao zinakuwa tayari kwenye mitandao hiyo.

Jumia Travel ni miongoni mwa mitandao hiyo ambayo inayo orodha ndefu ya hoteli takribani 1,500 za nchini Tanzania bara na visiwani ambazo zinaweza kufikiwa na watu wa ndani na nje ya nchi.

Hii ni fursa kwa wamiliki wa hoteli kuweza kutambua wateja wao ni watu wa aina gani na wanatarajia vitu gani kutoka kwao. Wateja wa sasa wanategemea kwa kiasi kikubwa kukuta taarifa zote kuhusu huduma za hoteli husika kuwepo kwenye mtandao na kupatikana mara moja pale wanapozihitaji.

Kwa bahati mbaya si hoteli na sehemu za malazi zote ambazo taarifa zake unaweza kuzikuta mtandaoni na hapo ndipo mitandao hii inapokuja kuziba hilo pengo.

Mitandao ya huduma za hoteli imekuja kuziba pengo lililokuwepo kwa muda mrefu baina ya watoa huduma hizo na wateja ambapo athari zilikuwa kwa pande zote mbili.

Wamiliki kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakikosa wateja wengi ambao wangeweza kuwafikia kwa njia ya mtandao kwa kutegemea ambao wanakwenda moja kwa moja na hivyo kupoteza mapato mengi. Na pia kwa wateja ambao walikuwa na shauku ya kujua sehemu husika kabla ya kwenda walikuwa wanakosa fursa hiyo kwa sababu hakukuwa na mbadala wa huduma hiyo. 

Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel (travel.jumia.com) ni mtandao nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao wenye orodha ya hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.

Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.

Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa).

Kabla ya mwezi Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas kama washirika wao katika masuala ya kifedha. 

No comments:

Post a Comment