Pages

Pages

Monday, November 07, 2016

Ridhiwan Kikwete naye amlilia mzee Samuel Sitta

Namkumbuka Mheshimiwa Samuel Sitta katika nafasi mbalimbali, kwanza kama kiongozi wa kisiasa.
Marehemu anaacha historia kubwa katika utumishi. Kumbukumbu inaonyesha amewahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali, itoshe kusema alikuwa kiongozi aliyethubutu matokeo chanya. Ameacha daraja la salenda na mabadiliko ya sheria mbalimbali akiwa wizara ya sheria.
Ridhiwan Kikwete pichani.
Marehemu amekuwa mbunge na spika wa bunge. Amekuwa mbunge wa Urambo toka 1975. Ameacha kumbukumbu ya kuenzi demokrasia na uwazi katika mijadala. Alilifanya bunge kuwa muhimili wenye nguvu na heshima kubwa sana mbele ya jamii. Aliliongoza bunge kujadili na kufikia maamuzi yale magumu na makubwa yaliyokabili serikali mfano wakati wa kashfa ya richmond.
Marehemu alikuwa mwenyekiti wa bunge lililotengenez rasimu ya pili ya katiba. Ameonyesha uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za utengenezaji wa katiba. Aliruhusu mijadala huru lakini pia hata palipotokea tofauti ya mitazamo aliziita pande hasimu na kujadili ili kupata muafaka kwa maslahi ya taifa letu.
Mheshimiwa sita amekuwa kama mzazi kwangu. Alikuwa anapata nafasi kunishauri na hata kunielekez nn nikifanye. Alikuwa mkali na asiyependa kuona mambo yanaharibika. Nakumbuka kipindi cha bunge la katika alitusimamia mimi na wenzangu kuhakikisha tunamaliza kazi ya kukusanya maoni ya jumla ili kuifanya kazi iwe rahisi kwa sekretariet.

No comments:

Post a Comment