Pages

Pages

Sunday, November 06, 2016

Kampeni ya Mtoto wa Kitaa wilayani Temeke yazinduliwa rasmi

Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Temeke, Hija Kipeleka akizindua rasmi kampeni ya Binti wa kitaa katika Wilaya ya Temeke, ambapo aliwashukuru wanaoendesha kampeni hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa CVIF George David  Maarufu kwa jina la Ambassador Angelo akielezea kwa kina kampeni ya Binti wa kitaa ilivyo wasaidia mabinti wengi na kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kampeni hiyo ambapo kwa sasa inaendelea kuzinduliwa katika Wilaya zilizopo jijini Dar.

Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Tandika Bi. Rauva Maulid akieleza namna akina baba walivyo na tabia ya kuwarubuni mabinti wenye chini ya umri wa miaka 18 na kuwababishia Mimba,na kuongeza kuwa kwa tandika watoto wengi wanapata mimba wakiwa na miaka kuanzia miaka 12.
Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Said Mgeni akisisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa jirani na watoto wao ili waweze kuwa rafiki na kuwaeleza matatizo wanayoyapata kwa sababu kwa kufanya hivyo mabinti watakuwa huru kueleza matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la mimba.
Aisha mkazi wa Tandika akieleza namna vijana wanavyowarubuni na kuwasumbua ili waweze kushiriki nao katika ngono uzembe.
Mkazi wa Mtaa wa Sheraton Tandika Fatuma akieleza namna baadhi ya mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 wanavyopata mimba kutokana na kurubuniwa kufanya ngono uzembe na kuwapelekea kupata Mimba, na kuwasihi wasiwe wepesi kudanganyika na vijana.
 Binti huyu aliyetambulika kwa jina moja tuu Mwajuma akieleza alivyo achishwa shule akiwa kidato cha pili kutokana na kukosa fedha za masomo hivyo timu ya Binti wa kitaa kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Tandika kwa pamoja wameungana kumsomesha Binti huyo SIDO kwa kuwa anapenda kuja kuwa mfanyabiashara.
 Anaitwa Amani Muuza Juice ya Miwa maarufu mtaa wa sokoni akielezea jinsi Mimba za utotoni zinavyowaharibia maisha mambinti wenye  umri chini ya Miaka 18, na kuwasihi wananchi wote kuipa sapoti kampeni ya Binti wa kitaa
Muwezeshaji katika uzinduzi wa kampeni ya Binti wa Kitaa Zero akitoa elimu juu ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni
 Kampeni ya Binti wa Kitaa huwakutanisha Mabinti pamoja na watu wa rika zote, hapa Msema chochote Steven Mfuko  maarufu kwa Jina la Zero akiwa na Bibi Zakia Seif akiwafunda mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 kutokuwa na papara ya kukimbilia katika ngono.
 Mmoja ya wageni waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa Jesca Kitomary alishauri kuwa wazazi wanatakiwa kuwaelimisha mabinti wao juu ya athari za mimba za utotoni  na kuolewa mapema, kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata mimba na kuolewa kwa muda.
 Meneja wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James kutoka kikundi cha wanawake Ma Injinia Tanzania akitoa shukurani kwa wote waliofika katika kufanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa kitaa katika  Wilaya ya Temeke
 Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa kitaa Temeke
 Wakiendelea kufuatilia kwa makini masomo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Binti wa kitaa
Baadhi ya watu zaidi wakiwa katika pande mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya Binti wa Kitaa. 
Baadhi timu ya Binti wa kitaa pamoja na wakazi wa Tandika wakiwa katika picha ya pamoja
Picha na Fredy Njeje.

No comments:

Post a Comment