Pages

Pages

Friday, April 22, 2016

Wananchi wa jimbo la Handeni wamlilia Waziri wa Maji

Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAZIRI  wa maji  Mhandisi  Gerson Lwenge, pichani juu ameombwa  kuingilia kati  na  kushughulikia  kwa haraka  utata  uliogubika  utekelezaji  wa mradi  wa  Bwawa  la maji  la malezi  lilipo kata  ya Malezi ,Mjini Handeni  ambao  haujaanza  licha  ya Benk ya Dunia  kutoa shs. Milioni 700  kwa  ajili  ya mradi huo.
Wakizungumza katika mahojiano na wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo, wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia maji  katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni sababu ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo kutolewa.
Kitombo alisema kwa taarifa alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo ambao  unatarajiwa  uwanufaishe Wakazi Zaidi  ya 6000. Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880. 
Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha zilizoingizwa katika akaunti ni shs. Milioni 700
Pia alieleza mshangao wake kwa nini mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.

(Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini,Omari Kigoda)
Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyoya Malezi. Muhaji Ramadhani Mlaki alisema kuwa mara nyingi amepokea wataalamu ambao wanakuja kuona eneo lakini hakuna kinachoendelea baada ya hapo licha ya kuwaambia watu wenye maeneo yao ambayo yameingizwa kwenye mradi huo waache kulima.
“Tunapata lawama kwa wananchi kwa sababu tunawalewesha hadi mwisho wanatuambia kuwa na sisi tumekuwa wanasiasa,” alisema.
 Naye Cecilia Ibrahimu wa Malezi Kwedinguzo ambaye ana shamba kwenye eneo hilo la mradi wa bwawa alikubali kutoa eneo lake kwa sababu maji ni kero inayowagusa watu wote. “Sina cha kusema nataka maji tu. Cha ajabu tuliambiwa tutapewa mashamba na kusaidiwa kulimiwa lakini mpaka sasa hatujaonyeshwa mashamba na mradi haujaanza,’ alisema Bi. Cecilia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata hiyo, Mzee Abdallah Kombo walipoingia katika uongozi kilio ni hicho hicho hadi hivi sasa. Alisema kuwa wananchi wanategemea malambo madogo yaliyochimbwa kwa juhudi za Mbunge wa zamani wa Handeni, marehemu Abdallah Kigoda.

No comments:

Post a Comment