Pages

Pages

Tuesday, January 05, 2016

Rais Dr John Magufuli apokea hati za utambulisho za mabalozi watatu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo 05 Januari, 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, tukio ambalo limefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mabalozi ambao wamekabidhi hati zao za utambulisho ni Balozi wa Jamhuri ya Korea Mheshimiwa Song Geum-young, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Mheshimiwa Roeland Van de Greer na Balozi wa Palestina Mheshimiwa Hazem M. Shabat.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti, Rais Magufuli amewapongeza kwa kuteuliwa kuja kuziwakilisha nchi zao hapa nchini, na amewaahidi kuwa serikali yake itatoa ushirikiano kwao ili shughuli zao ziweze kufanikiwa. 

Aidha, Rais Magufuli amesema Tanzania inatambua matokeo ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo na amewahakikishia mabalozi hao kuwa ushirikiano huo utaendelezwa kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wao Mabalozi waliokabidhi hati zao za utambulisho wamempongeza Rais Magufuli kwa uongozi mzuri alioanza nao tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wamemuahidi kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano hususani katika shughuli za maendeleo
©Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
05 Januari, 2016

No comments:

Post a Comment