Pages

Pages

Monday, January 11, 2016

 
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS



 Na Mwandishi Wetu

BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebela, January 30 katika Ukumbi wa Sativa uliopo Kyela, mkoani Mbeya, mpambano huo wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa huo

Akisaini mkataba huo mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa, amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito huo



Mchumiatumbo alisema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi mazito chini ya kocha wake 
Juma Urungu 'Mkebezi' 


ambapo kwa siku amekuwa akifanya mazoezi mara mbili au tatu kwa ajili ya kujiandaa na mpambano uho

nae Rais wa  TPBC Chaurembo Palasa ameongeza kwa kusema chama chao kimejizatiti kuinua mchezo wa ngumi kwa kufata taratibu na sheria za mchezo uho wa masumbwi nchini

kwanza wata akikisha kila bondia anapima afya na uzito wake kwa usalama wa mabondia wenyewe na usalama wao wawapo mchezoni

aliongeza kwa kusema kuwa watapima afya siku tano kabla ya mpambano huo ili kujilidhisha na afya za mabondia hawo wenye uzito wa juu nchini ambapo mabondia hawo wamekuwa adimu sana hapa nchini

No comments:

Post a Comment