Rungu la Dr Magufuli latua tena Bandari, Bodi ya Bandari yavunjwa, mwenyekiti wake atimuliwa, Katibu Mkuu Uchukuzi naye afutwa kazi
HALI imezidi kuwa tete kutokana na joto kali linalozalishwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli, baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusema kuwa Rais Magufuli amevunja bodi ya Bandari na ametengua nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi Profesa Joseph Msamichaka. Pia amefukuza kazi watendaji wote waliohusika na kupokea na kutoa makontena kwenye bandari kavu ICD' pamoja na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka baada ya kushindwa kusimamia fedha za TRL kiasi cha Sh Bil 16.
No comments:
Post a Comment