Pages

Pages

Thursday, December 10, 2015

RC Makalla awashukuru wana Kilimanjaro kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi, ataka kila Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa usafi

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla, amewapongeza wakazi na wananchi wake katika mkoa huo kwa kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli la kufanya usafi na kutunza mazingira katika siku ya Uhuru, 9 Desemba iliyoadhimishwa jana nchini kote.  
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla juu na chini mwenye miwani akishiriki kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru, yaliyoadhimishwa jana nchini kote.
Kwa kupitia siku hiyo, RC Makalla ameagiza wakazi wake na wananchi kuitumia kila siku ya Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa ajili ya mwendelezo wa kufanya usafi ili kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa safi.

Akizungumza jana mkoani Kilimanjaro, RC Makalla alisema kwamba wananchi wake walijitokeza kwa wingi kufanya usafi, huku akiwataka waendeleze kasi yao ya kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa safi. Alisema kwa kufanya hivyo si tu mkoa wao utakuwa safi, ila hata suala la magonjwa ya miripuko linaweza kuwa hadithi kutokana na kutunza mazingira yao. “Jana nilishirikiana kwa pamoja na wananchi wangu kufanya usafi, huku nikifanya usafi soko la Memorial, Hospitali Mawenzi na Soko la Marangu.

“Pamoja na kujitokeza huko kwa wananchi, naomba suala hili liwe jadi yetu kuanzia ngazi ya kaya, mtaa, kitongoji na katika maeneo yote,” alisema. RC Makalla aliagiza Halmashauri zote kuhakikisha masoko yote yanakuwa safi na takataka zinazolewa kwa wakati, bila kusahau mitaro.

No comments:

Post a Comment