Pages

Pages

Thursday, December 03, 2015

Mabondia Francis Cheka na Thomas Mashali kuzipiga Morogoro Desemba 25

Mabondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakiangaliana kwa usongo wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro. Picha na SUPER D BOXING NEWS


 Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitambiana mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro. Picha na Suped D

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Thomas Mashali wa Dar es salaam na Fransic Cheka wa Morogoro wamendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro uzito wa kg 76
akiongea na waandishi wa habari Mashali amesema kuwa hii ni vita ya Dar na Moro  hivyo kawaomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi wa Dar es salaam waweze kuhamia morogoro kwa muda kwa ajili ya kumsapoti
siku hiyo ambayo kwake atakuwa na kibaruwa kigumu ambapo atapigana na Cheka pamoja na wakazi wa Morogoro.

Bondia Chaka alijibu mapigo hayo kwa kusema siku zote anamweshimu bondia anaetaka mpambano wa marudiano hata hivyo dozi ya mashali ipo pale pale na nitampiga katika raundi za awali tu kwa kuwa nipo vizuri na naendelea na mazoezi.

Nae kocha wa Mashali Ramadhani Uhadi amesema kuwa cheka ni bondia wa kawaida sana hivyo wapenzi waje waone mchezo mzuri utakaochezwa na Mashali atakavyo msambalatisha Cheka siku hiyo mjini Morogoro
na kocha wa bondia Cheka Abdallah Salehe amesema Cheka yupo vizuri sana kwa sasa nimempika ameshaiva ata kama mpambano utakuwa leo Mashali atapigwa mapema sana.

Katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atapambana na Twaha Kassimu kg 63 na Vicent Mbilinyi kg 63 atakumbana na Deo Njiku wakati Pius Kazaula kg 66 atamenyana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Epson John  kg 57 na Sadiq Momba na wana dada Lulu Kayage kg 51 atapambana na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa.





No comments:

Post a Comment