Pages

Pages

Monday, November 23, 2015

UNIDO yapiga jeki viwanda vidogo vya mafuta ya alizeti mkoani Dodoma

IMG_2196
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga akitoa maelezo jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi zake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (kulia) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. 

Na Mwandishi wetu
Kutoratibiwa kwa mbegu za alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika kuendesha viwanda vyao kwa gharama nafuu. Hayo yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez.

Mratibu huyo alikuwa Dodoma kwa shughuli mbalimbali za ukaguzi wa miradi pamoja na kuhudhuria shughuli za bunge la Tanzania lililomalizika jana. Timothy alisema kwamba pamoja kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa mbegu za kutosha nchini Tanzania,hali halisi inayoelezwa na wasindikaji inaashiria kwamba sekta hairatibiwi vyema kwani wasindikaji hukaa muda mrefu bila kuwa na mbegu za kusindika.

Aidha alisema kwamba mbegu za alizeti zinazovunwa kuanzia Aprili hadi Julai na huwa na bei nafuu kipindi hicho lakini kama wasindikaji wakikosa mitaji na kununua mbegu chache, msimu unapoisha hawawezi tena kuendelea kufungua viwanda vyao.
Alisema kwamba wasindikaji hao wanakumbana na kiwango kikubwa cha riba kuanzia asilimia 20 kwenda juu , riba ambayo inakwamisha maendeleo ya viwanda hivyo.

IMG_2202
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa pili kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (wa pili kulia) wakipata picha ya ukumbusho katika matanki ya kuhifadhia mafuta ya alizeti kiwandani hapo.

Hata hivyo alipoulizwa wanafanya nini katika kusaidia wasindikaji hao kukabiliana na hali hiyo alisema kwamba kupitia kongano hilo na Shirikisho la wasindikaji wadogo wa alizeti kanda ya mashariki na kati (CEZOSOPA). wana mipango ya kuwezesha wasindikaji hao kuwa na nguvu katika soko na kuwa na uwezo wa kupata mitaji bila gharama kubwa.
Aidha kupitia kongano hilo chama hicho kitawezeshwa uboreshwaji wa viwanda vya wanachama wake ili viweze kushindana na kukidhi viwango vya Shirika la Viwango nchini Tanzania (TBS).
Wakala huyo alisema hayo katika mahojiano yaliyofanyika kufuatia ziara ya mradi wa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez kwenye kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya Dodoma, kinachonufaika na mradi wa ubia wa uboreshaji viwanda kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Wizara ya Viwanda na Biashara (TIUMP).
Kwa mujibu wa taarifa ya UNIDO, taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa inachangia kuimarika kwa sekta ya viwanda vidogo na vya kati vya usindikaji mafuta na kuviweka katika ushindani.
Aidha kupitia UNIDO ni viwanda hivyo vinawekwa katika hali ya kukua kuwa viwanda vikubwa.
IMG_2212
Mfanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Alpha Manyanga akiwa kwenye mashine ya kuchujia mafuta kiwanda hapo.
Katika ushirika wa aina hiyo ni matarajio ya mradi huo kufanikisha juhudi za kupunguza umaskini kama moja ya malengo ya maendeleo endelevu yanayotarajiwa na dunia.

Aidha katika upunguzaji huo wa umaskini mradi utachangia ongezeko la fursa za ajira na ukuaji wa uchumi.
Mkoa wa Dodoma wenye viwanda vya kusindika mbegu za alizeti vinavyofanyakazi katika mkaazi wakitumia zana dhaifu na vifungashia visivyokuwa na ishara yoyote ile na kuuza bidhaa zao kando mwa barabara wanahitaji mfumo thabiti wa ukuzaji wa shughuli zao na kueleweka.
Kutokana na mazingira hayo wajasirimali hawa hujikuta wakiingia hasara kubwa kwa kupoteza tija na pia soko lenye uhakika.
Kutokana na madhara hayo na pia kukosa hati ya ubora kwa kukosa mazingira yanayoruhusu hati hiyo kutolewa, TIUMP imelenga kusaidia wasindikaji hawa na teknolojia sahihi inayohitajika ili watoke pale walipo na kuwa na viwanda vidogo au vya kati.
Ingawa kwa sasa UNIDO inasaidia viwanda vinane vya mbegu za alizeti ili kuweza kuboresha bidhaa zao na utendaji kuna muonekano wa maendeleo makubwa siku za usoni hasa kwa wanachama wa CEZOSOPA ambao wameuinganishwa pamoja kwa ajili ya misaada mbalimbali ya kuwawezesha kuwa washindani katika soko.
IMG_2216
Mtaalamu wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (aliyeipa mgongo kamera) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (kulia) walipokua wakikagua mtambo wa kusafisha mafuta (Semi re-finery) uliofadhiliwa na UNIDO kiwandani hapo.

UNIDO wanatumia maarifa waliyojifunza Ethiopia kuimarisha wanachama wa CEZOSOPA ambao tayari wamekubali kuunda kampuni ya pamoja na kuwekeza katika kitu wanachokifanya kwa pamoja kwa lengo la kuongeza uwezo na ushindani katika soko.
Halmashauri ya Chamwino tayari imekubali kuipa ardhi CEZOSOPA kwa ajili ya uwekezaji huo mkubwa.

Aidha UNIDO imewezesha kupatikana kwa teknolojia rahisi kwa ajili ya usafishaji wa mafuta ya alizeti na teknolojia hiyo inafanyiwa kazi na VETA.
UNIDO wamesema teknolojia hiyo hiyo inasaidia kuweka mafuta katika viwango vinavyotakiwa kitaifa na kimataifa na kwamba teknolojia hiyo tayari inafanyakazi nchini katika viwanda viwili na vingine saba vimeonesha nia ya kupata teknolojia hiyo.
Imeelezwa kuwa fedha za mradi huo zinapatikana kutoka UNIDO na wadau wengine kama SIDA na UNDAP.
IMG_2233
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto akipozi kwa picha.
IMG_2237
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akifurahi jambo alipokuwa akipewa maelezo na Mtaalamu wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (kulia) ya mtambo mahususi wa kusafisha mafuta (Semi re-finery) uliofahdhiliwa na UNIDO.
  IMG_2252
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (wa pili kushoto) akimuongoza Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe wake kukagua mradi huo unaofadhiliwa na UNIDO.
IMG_2324
Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy akizungumza na waandishi wa habari nje ya kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya Dodoma.

No comments:

Post a Comment