Pages
▼
Pages
▼
Tuesday, November 17, 2015
Miriaam Odemba kuwa jaji maalum shindano la Miss Universe
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Maandalizi ya fainali ya shindano la Miss Universe Tanzania 2015 bado yanaendelea Mwanamitindo wa Kimataifa Miriam Odemba atakuwa jaji maalum katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mrembo wa Miss Universe anzania 2015. Majaji wengine watakaoshiriki katika kumtafuta mnyange wa mwaka huu ni Sheria Ngowi, Maria Sarungi Tsehai, Mariam Ndaba na Priyal wa sia couture.
Zoezi la usaili limeshakamilika na hatimaye kupata warembo watakaojiunga na kambi ya Miss Universe kesho siku ya jumatano kabla ya fainali tarehe 20 mwezi huu.
Warembo waliobahatika kuingia kambini ni 14 tu, majina na mikoa waliyotoka kwenye mabano Mariam Isack (Dar es salaam), Lilian Luth(Dar es salaam), Stacey Sulul(Dar es salaam),Willice Donard(Dar es salaam),
Lorraine Marriot(Dar es salaam), Dalena David(Dar es salaam), Mercy Zephania(Dar es salaam), Dinnah Kaijage(Dar es salaam), Melody Typhone(Dar es salaam), Joselyn Mirashi(Arusha), Nancy Matta(Mbeya),
Christina Shimba(Iringa), Belinda (Mwanza).
Mwaka huu Miss Universe imefanya usaili katika mikoa sita tofauti ikiwamo Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment