Pages

Pages

Tuesday, October 13, 2015

Mwili wa marehemu Dr Abdallah Omary Kigoda kuwasili kesho tayari kwa maziko wilayani Handeni, mkoani Tanga

MWILI wa marehemu Dr Abdallah Omary Kigoda aliyefariki jana nchini India katika Hospitali ya Apollo unatarajiwa kuwasili kesho Jumatano tayari kabisa kusafirishwa nyumbani kwao wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa mazishi.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na familia ya Dr Kigoda aliyekuwa mbunge wa Handeni na Waziri wa Viwanda na Biashara zinasema marehemu atazikwa Alhamis, kama ratiba itafanyika kama ilivyopangwa, ikiwa ni siku moja baada ya kifo chake.

Kwa jijini Dar es Salaam, msiba wa Dr Kigoda upo nyumbani kwake Upanga, mtaa wa Mindu, huku taratibu zote za msiba huo zikifanywa na ofisi ya Bunge.






No comments:

Post a Comment