Pages

Pages

Sunday, October 04, 2015

Kampeni za Uchaguzi jimbo la Chumbuni zapamba moto



Msoma Utenzi akisoma Utenzi maalum wakati wa Uzinduzi wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja uliofanyika katika Viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Zanzibar.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akiwa katika viwanja vya mkutano akishangilia na Picha ya Mgombea wake wa Ubunge kupitia CCM Ndg. Ussi Salum Pondeza AMJADI wakati wa mkutano huo
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Unguja.
Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakiwapungia mikono Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni wakati msoma utenzi akitaja majina ya Wagombea.
Wanachama wa CCM wa Tawi la Masumbani Jimbo la Chumbuni wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni Unguja
Mgombea Ubunge Jimbo la Mfenesini Kanali Mstaaf Masoud akimtunza msoma Utenzi wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa Jimbo la Chumbuni Unguja. 
Katibu wa CCM Jimbo la Chumbuni akisoma utaratibu wa mkutano huo wa kampeni wa jimbo hilo. 
Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Unguja Mhe Machano Othman, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo hilo na kuwaombea Kura Wagombea wote wa CCM wanaogombea katika Jimbo la Chumbuni kuazi Mbunge Mwakilishi na Madiwani kuwa kura ya Ndio kuendelea maendeleo katika jimbo hilo walioyawacha wao.kwa sasa anagombea Jimbo la Mfenesini nafasi ya Uwakilishi 
Mgombea Ubunge Jimbo la Mfenesini Kanal Mstaaf Masaud, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Uzinduzi ya Jimbo zilizofanyika katika viwanja vya mpira mabanda ya ngombe chumbuni Unguja. 
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Haji Ameir akizungua mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja uliofanyika katika viwanja vya mpira mabanda ya ngombe chumbuni na Kuwatambulisha Wagombea wa CCM wa Jimbo hilo.na kuwaombea Kura siku ya Uchaguzi Mkuu kwa kura ya Ndio, pamoja na Rais wa Zanzibar Dk Shein, na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya Kampeni wakishangilia na Vipeperushi vya wagombea wa Jimbo la Chumbuni Unguja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Haji Ameir akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza AMJADI, wakati wa mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni uliofanyika katika viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza Amjadi akiwataka Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kujiandaa na Maendeleo katika Jimbo hilo katika kipindi chake cha miaka mitano kuweza kulibandilisha Jimbo hilo katika maendeleo kwa Vijana na Wazee katika sekta mbalimbali zikiwemo za Elimu, Maji, Kujiajiri Wenyewe na Afya. amewataka kumpigia Kura ya Ndio kuweza kuwaletea maendeleo hayo. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni akimwaga Serazake kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya mpira mabanda ya ngombe chumbuni Unguja.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja wakati akihutubia Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Ussi Salum Pondeza AMJADI, uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni Unguja.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifuatilia Mkutano wa Kampeni wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraj Kwaza akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Unguja wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo na kusoma baadhi ya vipengele vya Ilani ya Uchaguzi ya CCM jinsi itakavyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya Dk Shein. 

Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Jimbo la Chumbuni Unguja



 Msanii wa Bendi ya Yamoto, akitoa burudani kwa Wanachama wa CCM wa Jimbo la Chumbuni wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo hilo.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Jimbo la Chumbuni Unguja
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Haji Ameir, akimtambulisha Mgombea Udiwani wa Wadi ya Chumbuni, Ndg. Mussa Haji Idrisa kwa Wananchi  wa Jimbo hilo 
Mgombea Udiwani Wadi ya Chumbuni Ndg Mussa Haji Idrisa. akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.
Mgombea Udiwani Wadi ya MuembemakundiNdg Haji Juma, akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.
Mgombea Udiwani Wadi ya MuembemakundiNdg.Haji Juma.  akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.



No comments:

Post a Comment