Pages

Pages

Friday, September 11, 2015

UNESCO yakabidhi kitabu cha mafunzo ya TEHAMA nchini

IMG_8554
Mkuu wa Ofisi  na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi  wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekabidhi rasmi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakuf unzi  wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyohudhuriwa na wadau walioshiriki katika uandazi wa kitabu hicho, ikiwamo serikali ya China.

Kitabu hicho ni matokea ya mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia. Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama  na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza. Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
IMG_8742
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kilichoandaliwa na mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China.

Akipokea kitabu hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome, Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa ameishukuru UNESCO na serikali ya China ya kuwezesha upitiaji wa kitabu hicho kinachotoa mwelekeo wa mafunzo ili kuambatana na maagizo ya viwango yaliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),

Alisema kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa utekelezaji wa elimu ya Tehama kwa kuzingatia uwezo na weledi katika ufundishaji. Kamishina huyo amesema kwamba kazi ya kuangalia viwango hivyo iliyofanywa kutokana na Mfuko wa China na Unesco kwenye moduli sita za uelewa na elimu ya teknolojia kwenye Tehama. Alishukuru timu iliyopitia viwango hivyo na kusema serikali ya Tanzania inashukuru msaada huo wa Unesco na serikali ya China kwa kufanikisha kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.
IMG_8684
Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun akitoa salamu za Balozi wa China nchini kwenye hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi  wa vyuo vya ualimu  na walimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Ni matumaini yake kwamba sasa Tanzania ina kielelezo cha kufuatia katika kufanikisha maandalizi ya walimu wenye weledi na uwezo katika kufundisha na kutumia teknolojia ya Tehama.
Naye Mkuu wa ofisi  na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues  akizungumza kabla ya kukabidhi kitabu hicho alisema UNESCO itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuimarisha elimu ya Tehama ili kufungua njia pana zaidi ya maendeleo.
Aidha ameikumbusha serikali ya Tanzania kutumia vyema kitabu hicho katika kuhakikisha kwamba mafunzo ya kariba ya hali ya juu yanatolewa ili kuwa na mafanikio makubwa katika sekta zote za elimu na teknolojia.
Alisema kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa hatua kwa hatua katika mafunzo ya Tehama na namna ya kufanikisha katika kumwelimisha mwanafunzi na vitu vinavyoweza kufanywa ili kuhakikisha kwamba elimu sahihi inawafikia wahusika.
Naye Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing kupitia kwa Ofisa wa Ubalozi Liu Yun aliyefika kwenye hafla hiyo,  alisema kwamba serikali ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha elimu ya Tehama nchini.
Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alishawahi kusikika akisema utoaji wa mwongozo huo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa katika mradi.
IMG_8806
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akielezea maandalizi na hatua walizopitia katika uandaaji wa kitabu hicho mpaka kukamilika kwa wadau wa sekta ya elimu walioshiriki hafla hiyo.
IMG_8817
Meza kuu ikimpongeza Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (hayupo pichani).
IMG_8926
Mkuu wa ofisi  na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akimkabidhi Kamishna wa Elimu, Prof.Eustella Bhalalusesa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China. Mradi huo una lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
IMG_8931
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa (walioketi kushoto) na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki kuandaa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wakati hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Mradi huo una lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
IMG_8734
Pichani juu na chini baadhi ya wadau wa sekta ya elimu na maafisa wa Shirika la UNESCO waliohudhuria halfa ya makabidhiano ya mwongozo wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi  wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye hoteli ya Protea Courtyard.
IMG_8811
IMG_8743
IMG_8510
Mkuu wa ofisi  na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akijadiliana jambo na Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
IMG_8766
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Elimu nchini mara baada kupokea kitabu cha mwongozo wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wakati hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho kilichokabidhiwa kwa Kamishna wa Elimu nchini katika hoteli ya Protea Courtyard Hotel jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment